Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, pia umetoa fursa kwa baadhi ya
wajasiriamali kuutumia kufanya biashara. Hili ni moja ya mabanda kwenye
Viwanja vya Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma
Mtangazaji wa Uhuru FM, Steve Mhina akimhoji Mhariri wa gazeti la
Mzalendo, Bakari Mnkondo kuhusu yanayojiri kwenye banda la Kampuni ya
Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na
Burudani, ambalo limo kwenye viwanja vya Kizota kuhajihisha mkutano huo
Mobu la Vijana kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar
es Salaam, wakiwa kwenye viwanja vya Kizota. Katibu Mkuu wa UVCM
Martine Shigela alikuwa mmoja wa wagombea wa NEC, Viti Kumi Bara
Watu wakifuatilia kwenye TV yaliyokuwa yakijiri ukumbini, wakiwa wameketi raha mustarehe nje ya ukumbi wa Kizota
Mamaaa Asha Baraka akitembelea banda la Uhuru Publications Ltd
'Wataalam' wa kuchoma nyama wakiwa kazini kwenye viwanja hivyo
Baada ya pilika pilika za kusaka kura kwa ajili ya wagombea wao, baadhi
ya wapambe wakijiliwaza kwa kiywaji kwenye mabanda yaliyopo katika
viwanja vya Kizota
Banda la maonyesho la Uhuru Publications linavyoonekana kwenye viwanja vya Kizota
Makada wa CCM, wakiwa nje ya viwanja vya Kizota kufuatilia hali ya
amambo Uwanjani. Kutoka kushotoKatibu wa CCM Nzega, Kajoro Vyohoroka,
Mwenyekiti wa CCM Nzega, Amos Kameda, Mjumbe wa NEC Nzega Yassin Memba
na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa CCM, Edward Mpogolo.
"TUPIGE NA SISI PICHA TUONEKANE" ni Mjumbe wa Mkutnao Mkuu (UWT) kutoka
Mara Agnes Mathew na Mjumbe wa NEC kutoka Katavi Kampala Maganga.
Mhariri wa Mzalendo, Bakari Mnkondo akiwa na wafanyakazi wenzake wa
Uhuru Publicatiosn Ltd Selina Wilson na Latifa Ganzel kwenye banda la
UPL kwenye Viwanja vya Kizota
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Frank akipata maelezo ya dawa
za maradhi mbalimbali za asili zinazouzwa na mjasiliamali Roda Forman
kutoka Mbeya kwenye viwanja hivyo vya Kizota
Picha na Daily Nkoromo.
Post a Comment