MBUNGE wa
Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha
ya vigogo walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina
hayo kama Serikali inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi
ambayo ilitajwa Mwembe Yanga bado haijashughulikiwa.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara jijini
Mwanza, Mnyika alisema kwamba kama Serikali ya CCM inasisitiza kutaka
majina ya walioficha fedha huko Uswiss yatajwe, wanapaswa kusimama na
kueleza ile orodha ya mafisadi ambayo Chadema waliitaja pale Mwembe
Yanga imefanyiwa kazi gani.
“Watu
wanapotutaka tutaje majina, na sisi tunawambia kwanza wasimame na
kutueleza ile ‘list’ (orodha) ya mafisadi ambayo tuliitaja kwa majina
wameishughulikia vipi?” alihoji Mnyika na kuongeza kwamba wanajua jinsi
ambavyo CCM wanalivyonufaika na ufisadi kupitia Kampuni ya Kagoda jambo
ambalo linadhihirisha kuwa haiwezi kuwa rahisi kwao kushughulika na vita
ya ufisadi.
Alisisitiza
kuwa wanaotaka majina yatajwe wanayo ajenda yao na wao wameshaifahamu
hivyo hawatashughulika nayo na kusema ukifika wakati ambao wao
wanautambua wataweka kila kitu nje, lakini siyo kwa kushinikizwa na
Serikali ya CCM.
“Tunajua
serikali hii inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi haina dhamira ya
kushughulika na ufisadi, na hili ndilo litakalowaondoa madarakani,”
alifafanua.
Hata hivyo
mkutano huo uliingia dosari wakati Mnyika akiendelea kuhutubia ambapo
mawe yalianza kurushwa na vijana wanaodaiwa kuwa ni vijana wa Diwani wa
Kata ya Kitangiri kwa tiketi ya Chadema, Henry Matata aliyevuliwa
uanachama.
Kutokana hali hiyo vijana wa Chadema walizungumza katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa vijana wawili ambao walishambuliwa na kueleza na kunusuriwa na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje aliyeita polisi na kuwaomba waache kuwashambulia.
Awali
akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Wenje
alieleza wananchi kuwa katika mkakati wake wa kuboresha elimu ya msingi
na sekondari amefanikiwa kutengeneza madawati mengine 400 baada ya
madawati ya awali 500 kugawiwa katika shule.
Alisema
madawati hayo yatagawanywa kwa shule 30 za wilaya ya Nyamagana na
kubainisha kwamba kutokana na madaati ya awali 500 kutolewa bila
utaratibu na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,Wilson Kabwe hivyo madawati
haya alieleza kuwa yatasambazwa na madiwani wa Chadema katika shule
pamoja na katibu wa ofisi yake ili kuhakikisha yanafika katika shule
husika iliyopangwa.
Mwananchi
Post a Comment