Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha
Makutano, Magic FM
Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka
kwa Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango
Mbunge wa Kigamboni akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na
wasikilizaji wa Kipindi cha Makutano.
Picha na Makutano Show-
-
Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine
Ndungulile amesema
kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali
imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi juu ya mradi wao. Mheshimiwa Ndugulile
ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi
huo katika
kipindi cha Makutano, Magic FM.
Mradi
huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala
mkubwa kwa
wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao
vya
bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo.
Alisema
tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria inayotaka
ushirikishwaji wa wananchi kila
hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi
wanataka
majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa
kuhusu
fidia.
Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo
lake uliosababishwa na wao kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko
wa
waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa
kwa sasa
umeisha na kila mmoja ameshajua kosa lake.
Via Hakingowi Blog
Post a Comment