Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TAA ZA BARABARANI JIJINI MBEYA ZAZIDI KUGONGWA NA MAGARI KILA KUKICHA

Gari aina ya Coster ambalo leo alfajiri limeparamia nguzo mbili za taa za barabarani eneo la Barabara Kuu iendayo Zambia na kung'oa nguzo hizo kisa kikiwa ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa na haraka ya kuwahi abiria katika kituo cha abiria cha Mwanjelwa na Uyole Jijini Mbeya.
Nguzo ikiwa imelala chini baada ya kuparamiwa na gari ya abiria liyekuwa kuwa mwendo kasi hivyo kukosa muelekeo na kusababisha kisa hicho.
Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya uharibifu wa nguzo hiyo na basi lililogonga nguzo hiyo.

Kumekuwepo na kutupiwa lawama kwa madereva wa magari pamoja na boda boda kutojali sheria za usalama barabarani hali inayo changia uharibifu wa mali na pamoja na kupoteza uhai wa watu.Hali hiyo imechangiwa na madereva hao kutumia kinywaji kinywaji kikali maafuru kama viroba wawapo kwenye kwenye gari wakiendesha ambacho huweka kwenye chupa ya maji ili kuwazubaisha watu wadhani dereva anakunywa maji kumbe ni kilevi hicho.(SOMA:Madereva huendesha wakinywa ‘viroba’ vya pombe katika chupa za maji safi

Dereva wa gari hiyo iliyosababisha ajali alikimbia baada ya ajali ili kukwepa mkono wa sheria na kuliacha gari hapo.

 Picha na Mbeya Yetu.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top