Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa Chuo), akisikiliza maelezo
ya maendeleo ya Jengo Jipya la Chuo Cha Usafirishaji(NIT) kutoka kwa Mkuu wa
Chuo hicho, Mhandisi.Dkt. Zacharia Mganilwa (aliyevaa suti ya Kaki), wakati
Waziri wa Uchukuzi alipotembelea Chuoni hapo jana kutunuku Stashahada za
Juu, Stashahada za Kawaida na Shahada mbalimbali katika mahafali ya 28 ya Chuo hicho,jana
mchana.
Mkuu
wa Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mhandisi, Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti
ya Kaki), akimuonyesha Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa
Mkuu wa Chuo), eneo ambalo Chuo kimelitenga kwa ajili ya wenye Magari
watakaomua kupaki magari yao na kwenda kutumia Usafiri wa Treni inayotoka
Ubungo kuelekea Stesheni jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mhandisi.Dkt. Zacharia Mganilwa(aliyevaa suti ya
Kaki), akimueleza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Kulia kwa Mkuu wa
Chuo), namna ambavyo Maktaba ya Chuo hicho inavyofanya kazi, chuoni hapo jana
Mchana. Dk Mwamkyembe alipita katika maeneo mbalimbali kabla ya kuhudhuria
mahafali ya 28 ya Chuoni hapo.
Baadhi
ya Wageni walioalikwa katika mahafali ya 28 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT), wakimsikiliza
Mgeni Rasmi Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe katika
Viwanja vya Chuo hicho.
Waziri
wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia wahitimu pamoja na Wageni
waalikwa katika mahafali ya 28 ya Chuo cha Usafirishaji(NIT), Mahafali hayo yamefanyika
katika Viwanja vya Chuo hicho jana Mchana, ambapo wahitimu wa Kozi mbalimbali walitunukiwa
Stashahada za Kawada, Stashahada za Juu na Shahada.
Waziri
wa Uchukuzi.Dk. Harrison Mwakyembe(Aliyevaa kofia Nyekundu),akiwa katika picha
ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka katika Chuo Cha Usafirirshaji(NIT),jijini Dar es Salaam.
Picha na mjengwa Blog
Post a Comment