 |
| Kaimu
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Longinus
Rutasitara (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na Wajumbe
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na wadau wengine (hawapo
pichani) kujadili misaada ya Serikali ya China katika kuisadia Tanzania
kutekeleza miradi mikubwa katika sekta kama vile Kilimo, Miundombinu na
Umeme. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka Tume hiyo. |
 |
| Balozi
Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mchango
wake wakati wa majadiliano na ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu
kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa. Wengine katika picha
ni Bw. Lin Zhiyong (katikati) Mwakilishi Mkuu katika masuala ya Uchumi
na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini na Bi.
Fang Wang, Afisa kutoka Ofisi hiyo. |
 |
| Bw. Lin Zhiyong akitoa maoni yake wakati wa majadiliano hayo. |
 |
| Balozi
Kairuki na wajumbe kutoka China wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji,
Bw. Rutasitara (hayupo pichani) wakati wa majadiliano. Wengine katika
picha ni Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na Tume ya Mipango walioshiriki mkutano huo. |
 |
| Bw. Rutasitara na Maafisa wengine wakimsikiliza Bw. Li wakati wa majadiliano hayo. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Monday, November 12, 2012
Post a Comment