Uongozi
wa klabu ya Young Africans umewapa mapumziko ya wiki mbili wachezaji
wake wote kufuatia kuwepo kwa mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom
iliyomalizika mwishoni mwa wiki na kuendelea tena mwakani mwezi Januari
2013.
Kocha Mkuu Ernest Brandsts amesema wameamua kutoa mapumziko hayo
kufuatia wachezaji hao kuwa na timu tangu mwezi wa nane wakati wa
maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom hivyo hawajapata nafasi ya kupumzika
na familia zao.
Young Africans imemaliza mzunguko wa kwanza kwa
kufikisha pointi 19, kufuatia kucheza michezo 13, imeshinda michezo 8,
imetoka sare michezo 2 na kufungwa michezo 2, aidha pia imefunga mabao
25 na kufungwa mabao 10.
Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Young
Africans anaongoza kwa kufunga mbao 8 sambamba na mchezaji Kipre
Tchetche wa timu ya Azam.
Wachezaji Kelvin Yondani, Frank Domayo,
Saimon msuva na Athumani Idd 'Chuji, wamejiunga na timu ya Taifa ya
Tannzania 'Taifa Stars' ambayo inacheza mchezo wa kirafiki na timu ya
taifa ya Kenya Harambee Stars katika mchezo huo uliopo katika kalenda za
FIFA.
Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite,Hamis Kiiza na Didier
Kavumbagu wanatarajiwa kujiunga na timu zao za Taifa katikati ya wiki
hii, kwa ajili ya maandalizi ya mashindano la TUSKER CECAFA Cup ambayo
mwaka huu yatafanyika nchini Uganda kuanzia Novemba 24.
Wachezaji
wote waliobakia ambao hawatajiunga na timu zao za Taifa watarejea klabu
tarehe 26 Novemba tayari kwa kuanza mazoezi tarehe 27 Novemba ikiwa ni
maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Chanzo:Young Africans
Post a Comment