(Picha na Princess Asia)
Na Princess Asia
KATIKA
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar
es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema
mwakani.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika
Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga
na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya
Desemba na Februari 25, mwakani.
Alisema
pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie
Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili
ya timu kuweka kambi.
Alisema
ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu
zitkazotajwa baadaye.
Aidha, kocha
mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya
miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.
Katika hatua
nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti,
Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa
kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu kuongoza.
Alisema kufanya
vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda
baada ya Kombe la Kagame.
Post a Comment