Tofauti ya kipato wakati mwingine si chochote linapokuja suala la Mpira wa Miguu .Kwa wale wafuatiliaji wa Kombe la Capital One jana Klabu ya Arsenal ilipotupia virago na kushindwa kuingia Nusu Fainali baada ya kutoshana nguvu ya goli 1-1 na baadae kuondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati Bradford 3-2 Arsenal.
Kibao kikionyesha majina ya wachezaji waliokosa na kupata penati zao kwa kila timu na kupelekea Arsenal kuondolewa katika mashindano hayo.
Ushindi huu umeshangaza kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati ya Bradford na Arsenal katika vikosi vilivyocheza kwenye michezo huo ambapo kikosi cha Arsenal kilichocheza mchezo huo ulikuwa na jumla ya thamani ya paundi 66.8Milioni huku waliokuwa wanacheza nao Bradford kikosi chao kilikuwa na jumla ya paundi 7,500 lakini wachezaji hao hawakujali kama wanacheza na mamilionea na kuwa ondoa kwenye Mashindano hayo.
Chanzo:Daily mail.

Post a Comment