Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BONGE LA STRAIKA KUTUA SIMBA KUMALIZA UKAME WA MAGOLI

  Umony
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MSHAMBULIAJI wa Uganda, Brian Umony amesema kwamba yuko tayari sasa kuchezea Tanzania kuchezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam, baada ya kushindikana mwaka 2009, alipokuwa KCC ya hapa.
 
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa baada ya kuiongoza Uganda kuifunga Sudan Kusini maao 4-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge, Umony alisema Simba kama wanamtaka wamfuate hata sasa wamalizane.
 
 
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
 
 
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa Sc Villa wakati huo.
 
 
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C.
 
 
Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu sawa na Suleiman Ndikumana wa Burundi na wao ndio wanaongoza kwa mabao, wakifuatiwa na John Bocco, Khamis Mcha, Chris Nduwarugira, David Ochieng na Clifton Miheso wenye mabao mawili kila mmoja.
 
 
Wengine wenye bao moja kila mmoja ni Yussuf Ndikumana, Mohamed Jabril, Geoffrey Kizito, Hamisi Kiiza, Robert Ssentongo, Yonatal Teklemariam, Haruna Niyonzima, Jean Mugiraneza, Dadi Birori, Ramadhan Salim, Gatech Panom Yietch Ethiopia, Farid Mohamed, Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone, Patrick Masanjala, Amir Hamad Omary na Yosief Ghide. 
 
 
Jumla ya mabao 32 hadi sasa yamefungwa katika mechi 20 za makundi yote matatu, zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.

WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
Suleiman Ndikumana   Burundi    3 (1 penalti)
Brian Umony                Uganda    3
John Bocco                  Tanzania  2
Khamis Mcha                Zanzibar  2
Chris Nduwarugira        Burundi    2
David Ochieng              Kenya      2
Clifton Miheso               Kenya      2
Yussuf Ndikumana        Burundi   1
Mohamed Jabril            Somalia    1(penalti).
Geoffrey Kizito              Uganda    1
Hamisi Kiiza                  Uganda    1
Robert Ssentongo         Uganda    1
Yonatal Teklemariam     Ethiopia    1
Haruna Niyonzima         Rwanda    1
Jean Mugiraneza           Rwanda    1
Dadi Birori                     Rwanda    1
Ramadhan Salim           Kenya       1
Gatech Panom Yietch    Ethiopia     1
Farid Mohamed              Sudan       1
Chiukepo Msowoya        Malawi       1
Miciam Mhone                Malawi      1
Patrick Masanjala           Malawi      1
Amir Hamad Omary        Eritrea      1
Yosief Ghide                  Eritrea      1(penalti).

Chanzo:BongoStaz Blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top