 |
| Afisa Uraghashi
na mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Ndugu
Philemona Marijani akitoa maelezo juu ya Banda la WAMA kwa Afisa
Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Lindi Ndugu Anna Maro katika maazimisho ya
Siku ya ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi, Leo Tarehe
01st December 2012. |
 |
| Wageni mbalimbali
pamoja na maafisa wa serikali ngazi mbalimbali mkoa wa Lindi wakiwa
mbele ya jengo la WAMA wakisubiri kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa
katika Banda hilo. Katika Maazimisho yaliyofanyika hii leo kitaifa
Mkoani Lindi. |
 |
| Afisa Uraghishi
wa Mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Ndugu
Philemona Marijani (wakwanza Kulia) akiwa na Afisa Tathmini na
Ufuatiliaji wa Taasisi hiyo Ndugu Gloria Minja (wa katikati) na Mwajuma
Lubu Muelimishaji wa Taasisi hiyo ya WAMA Mkoani Lindi. |
 |
| Wanawake na
Wananchi mbalimbali wa Mkoani Lindi wakiwa katika Banda la WAMA kupata
Huduma mbalimbali zinazotolewa katika Banda hilo, wa kushoto ni Zena
Tozo Muelimishaji Afya ya Msingi kwa Jamii kutoka Wilaya ya Bagamoyo
ambayo ni mmoja wa waelimishaji Afya wa WAMA katika kuzuia maambukizi ya
VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto. |
 |
| Katibu Mtendaji
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Ndugu Daud Nassib akiwa anagawa
fulana za Taasisi hiyo kwa Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi
waliohudhuria katika Maazimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika
Kitaifa Mkoani Lindi, leo tarehe 01 Dec 2012. |
 |
| Vicky Chuwa mmoja
wa maafisa wa UNICEF hapa nchini akiwa katika Banda la TACAIDS kwenye
maazimisho ya Siku ya Ukimwi iliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi. |
 |
| Jukwaa Kuu katika Uwanja wa Ilulu likiwa limepambwa tayari kutumika katika Maazimisho hayo. |
 |
| Wananchi
mbalimbali wa Mkoa wa Lindi wakiwa wamehudhuria na wengine wakiwa
wanaendelea kuhudhuria katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi, ambapo
yamefanyika Maazimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ukimwi Duniani. | |
Chanzo:CCM Blog
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Saturday, December 1, 2012
Post a Comment