Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Serikali ya Tanzania kuanzia Jumamosi (tarehe 1 Disemba) itaacha kutoa
leseni kwa makampuni binafsi ambayo yanaendesha mabasi ya usafiri wa
umma jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na
Nchi Kavu (SUMATRA) ilitangaza.
Ofisa wa trafiki akiongoza msongamano wa
dala dala kwenye barabara ya Uhuru katika eneo la Congo la Dar es
Salaam. [Deodatus Balile/Sabahi]
Pia serikali haitahuisha leseni zilizopo kwa magari binafsi ya usafiri,
hata hivyo, yataendelea kufanya kazi hadi vibali vyao vimalizike muda wa
matumizi, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Ahmad Kilima.
Waendeshaji wa mabasi ya usafiri wa umma ambao wanataka kufanya kazi
kama makandarasi wa serikali watapewa leseni za muda hadi mikataba
itakapoanza kutumika mwezi Juni 2013.
Harakati hii ni sehemu ya mpango mkubwa wa kubadilisha mabasi madogo na
mfumo wa mabasi ya umma yaendayo kasi unaosimamiwa na serikali. Serikali
inategemea mpango wa usafiri mpya kuboresha usafiri wa umma, ukipunguza
msongamano wa magari Dar es Salaam, ambapo SUMATRA inasema iliwagharimu
Watanzania kiasi cha shilingi bilioni 4 (dola milioni 2.5 ) kila siku,
kwa kuwa wasafiri wanapoteza muda mwingi kwenye msongomano wa magari.
Tangazo la Jumatano (tarehe 28 Novemba) lilikuja mwezi mmoja baada ya
serikali kuzindua mfumo wa kwanza wa usafiri wa reli ya umma wa mji huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam Cosmas Tekule
alisema usimamishaji wa kutoa leseni kwa takribani magari madogo 10,000
ya usafiri wa umma, yanayojulikana kama "dala dala", ulikuwa ni wa
lazima kwa sababu hayana uhakika na yanasababisha msongamano na
uchafuzi.
"Tunaleta mabasi makubwa ambayo yatabeba hadi abiria 150," aliiambia
Sabahi. "Kwa madaladala, yanayochukua abiria wapatao 30, unahitaji
magari madogo matano ya abiria kuingia katikati ya mji kuchukua idadi
hiyohiyo ya watu. Ni dhahiri, hii ni gharama kubwa."
Alisema matumizi ya mafuta pia yatapungua kwa mabasi makubwa, kupunguza
utoaji wa gesi ya kaboni, ambalo ni jambo zuri kwa mazingira. Mabasi
mapya yanatarajiwa kuhudumia kiasi cha abiria 800,000 kila siku.
Zaidi ya hayo, serikali inajenga upya barabara kadhaa na kuweka barabara ya magari yaendayo kasi kwa mabasi mapya.
Pontian Michael, mmiliki wa kampuni ya kuchomelea vyuma katikati ya
jiji, aliiambia Sabahi kwamba uondoaji kwa awamu wa daladala utaboresha
maeneo ya maegesho katika wilaya za biashara, ambayo alisema yamezuia
wateja wanaotarajiwa.
Maana ya hii kwa madereva wa dala dala
Lakini madereva walisema mfumo mpya wa usafiri wa umma utapelekea kupoteza kazi kwa wengi miongoni mwao.
Mohamed Ibrahim, ambaye amekuwa akiendesha katika jiji kwa miaka 22,
alisema wamiliki wengi wa mabasi ya usafiri wa umma ni wafanyabiashara
wadogo ambao hawawezi kushindana dhidi ya wafanya biashara wakubwa
kupata mkataba na serikali. "[Wamiliki wa makampuni makubwa] watawaajiri
ndugu zao na karibia madereva wote wa dala dala wataachwa bila kazi,"
aliiambia Sabahi.
Michael Kakele, mmiliki wa dala dala anayesimamia Kampuni ya Kakele
Transport, alisema kwamba waendeshaji binafsi wamekuwa katika mazungumzo
na serikali kuhusu kipindi hiki cha mpito tangu mwaka 2010, na
wanafurahia kufanya kazi katika muundo huu mpya.
Lakini aliiambia Sabahi itakuwa vigumu kumudu gharama za ununuzi wa
mabasi ambayo yatafikia viwango vipya, kwani yatagharimu hadi shilingi
milioni 250 (dola 160,000), ambazo wamiliki hawawezi kukopa kirahisi
katika benki. Serikali inaweza kuwasaidia wamiliki kupata mabasi na
kupata sifa za mikataba kama itatoa dhamana ya mkopo kwa angalau wale
wanaoendesha usafiri wa umma ambao walikuwa katika biashara kwa muda
mrefu, alisema Kakele.
Chanzo sabahionline.com/
Post a Comment