Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA ZAWADI TOKA LISBON URENO KWA MDAU

Ofisi za Kampuni ya Renex iliyopo Lisbon,RENEX ni Kampuni ya mabasi  nchini Ureno.Eneo la Kampuni hiyo linaonekana likiwa safi muda wote likiwa na vifaa vya kutupia taka na vyoo safi kwa wasafiri watumiao Mabasi hayo.Hali ni tofauti ukija hapa Nyumbani ambapo tumeshuhudia uchafu na kutojali afya za wasafiri hivyo mtu anapoamua kusafiri hupata shida kuanzia anapofika eneo la kupandia basi kutokana na mpangilio mbovu wa huduma mbalimbali kwa wasafiri.Haya tumekuwa tukiyashuhudia Kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani ikiwa ni pamoja na kulanguliwa tiketi.

Zawadi toka Lisbon, Ureno kuelekea Sikukuu za Christimas na Mwaka mpya kwa wale wasafiri.Suala la Usalama ni muhimu sana kwa wewe msafiri na ungependa usafiri kwa usafiri wa uhakika na salama.NImepiga picha hii ili kuwakumbusha ndugu jamaa na marafiki kuwa wanaposafiri hususani kipindi hiki cha Disemba suala la usalama ni muhimu sana hasa basi watakalopanda ili waweze fika salama.

Kipindi hiki huwa tunashuhudia baadhi ya wafanyabiashara ambao hawajali usalama wa abiria wakitoa mabasi yao gereji ili mradi tu avune pesa na kuwasumbua abiria kwa gari kuharibika mara kwa mara liwapo barabarani.


 
PICHA NA MDAU WETU

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top