DK 90:00 +4:43 Full time Full Time Everton 1 - 2 Chelsea
.
DK 87:58 Emboaba Oscar anapiga shuti langoni mwa Everton lakini linatoka sentimita chache na kuwa goli kiki
DK 85:47 Booking Refa anampa kadi ya njano mchezaji Ashley Cole.
DK 84:25 Substitution (Chelsea), Emboaba Oscar anaingia badala ya Juan Mata.
DK 81:44 Cesar Azpilicueta Anaingiza krosi , Phil Jagielka anaiondoa kwenye hatari
DK 79:48 Substitution Bryan Oviedo anachukua nafasi ya mfungaji wa bao Steven Pienaar.
DK 77:3 Ross Barkley anaingia badala ya Thomas Hitzlsperger.
Distin anazawadiwa kadi ya njano kwakucheza vibaya
DK 72:58 Mabadiliko Victor Moses anaingia badala ya Eden Hazard
DK 71:21 Goal LINAFUNGWA Frank Lampard - Everton 1 - 2 Chelsea Goli linafungwa na Frank Lampard kutoka ndani ya 18 kwenye kona ya kulia ya goli la Everton na hivyo Everton 1-2 Chelsea.
DK 70:10 Eden Hazard anamchezea vibaya Phil Jagielka. mpira wa adhabu unapigwa na Thomas Hitzlsperger, Fernando Torres anaokoa mpira huo kutoka eneo la hatari
DK 69:21 Booking David Luiz Anazawadiwa kadi ya njano
DK 66:21 Fernando Torres anapiga shuti langoni. Linaokolewa na Tim Howard. Na kuwa kona inayopigwa Juan Mata, Thomas Hitzlsperger anaokoa mpira huo. Kona tena inapigwa na Frank Lampard lakini kiulaini inaokolewa na Tim Howard.
DK 63:42 Booking Steven Pienaar anapewa kadi baada ya kumcheza vibaya David Luiz
DK 58:46 Kona inapigwa na Steven Pienaar langoni mwa Chelsea na Fernando Torres anaosha mpira ule.
DK 53:33 Fernando Torres anaingiza krosi maridadi , Thomas Hitzlsperger anaondoa mpira huo eneo la hatari
DK 52:07 Steven Pienaar anaingiza majalo moja , Frank Lampard anaosha pale kuondoa hatari langoni
DK 53:13 Krosi inaingizwa na Victor Anichebe,Ross Turnbull anaokoa mpira huo
DK 50:14 Kona inapigwa Eden Hazard karibu na mtambaa wa panya lakini, Nikica Jelavic anaondoa hatari hiyo
DK 47:21 Booking
Gary Cahill anazawadiwa kadi ya njano
DK 45:00 +1:22 Half Time Everton 1 - 1 ChelseaLampard akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake goli
DK 41:11Goal - Frank Lampard anaifungia Chelsea goli la kusawazisha - Everton 1 - 1 Chelsea .Nascimento Ramires anamtengenezea pasi maridadi
DK 37:53 Frank Lampard anapiga shuti lakini kiulaini Tim Howard anadaka shuti hilo.
Distin akichuana kuwani mpira na Ramires
DK 35:04 Krosi inaingizwa na Cesar Azpilicueta, Thomas Hitzlsperger anafanikiwa kuondoa mpira huo katika hatari
DK 30:28 Steven Pienaar anachonga kona maridadi kutoka kushoto na Fernando Torres anaokoa mpira huo .
Steven Pienaar akichuana vilivyo na David Luiz wa Chelsea
DK 27:00 Juan Mata anapiga shuti golini na linaokolewa na Tim Howard.
Dk 22:46 Krosi iliyopigwa na Fernando Torres, inaondolewa kwenye eneo la hatari na Phil Jagielka
DK 14:35 Gary Cahill ANACHEZEWA SIVYO NA Nikica Jelavic na hivyo adhabu hiyo inapigwa na Petr Cech kuelekea upande wa Everton
DK 8:33 Nikica Jelavic anamchezea vibaya Frank Lampard na kusababisha faulo inayopigwa na David Luiz.
Pienaar akipiga shuti na kutinga wavuni
Dk 1:02 Goal - Steven Pienaar anaifungia Everton goli hivyo kuipa timu yake goli la kuongoza - Everton 1 - 0 Chelsea
Post a Comment