Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TUME YACHUNGUZA KILIO CHA MAJI GOBA

Na Katuma Masamba
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini bado inafanyia kazi malalamiko  yaliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) anayetaka kujua kiini cha wakazi wa Goba kutokupata maji.

Mnyika aliwasilisha barua yake yenye malalamiko kwenye Tume hiyo ili kujua tatizo linalosababisha kata ya Goba kukosa huduma ya maji tangu mwaka 2007.

Mkurugenzi wa Tume hiyo ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora, Francis Nzuki alisema malalamiko hayo bado wanayafanyia uchunguzi ili kubaini tatizo linalofanya kata hiyo isipate maji kwa muda mrefu sasa.
Alisema baada ya kukamilika kwa uchunguzi watatoa majibu haraka iwezekanavyo juu ya malalamiko hayo ila kwa sasa bado wanaendelea kufanyia kazi malalamiko hayo.

Wakazi wa Goba wanalalamikia ukosefu wa maji unaowaathiri wakazi kwa muda mrefu sasa ambapo hulazimika kununua ndoo moja yenye ujazo ya lita 20 kwa Sh 500 hadi Sh 700.

Naye Mnyika alisema amekuwa akijitahidi kufanya juhudi ili wapiga kura wake waondokane na tatizo hilo na kuongeza kwamba Halmashauri ya Kinondoni ndiyo inayokwamisha kata hiyo isipate maji.
Mnyika alisema anaendelea kusubiri taarifa itakayokuwa na majibu ya malalamiko yake ili ajue tatizo liko wapi kwa wananchi kukosa maji miaka yote hiyo.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top