Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAKUBWA HAYA:WANAFUNZI ARU WAANDAMANA KUPINGA KUZUIWA KUVAA NGUO FUPI,KUBANA

Wanafunzi  wa kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi (Aru), kilichopo jijini Dar es Salaam wameandamana mpaka ofisi ya serikali ya wanafunzi kupinga tangazo lililobandikwa chuoni hapo linalowataka kuanzia kesho wasivae nguo fupi na za kubana.

Tangazo hilo lilibandikwa Alhamisi wiki iliyopita, saa 10 alasiri, likiwa na maandishi yanayosomeka: “kuanzia tarehe 1 mwezi wa kwanza hakuna mwanafunzi yeyote kuvaa nguo fupi na za kubana. Tunashukuru uongozi wa wanafunzi kutekeleza hilo kwani tulisikia katika vyuo vingine sasa zamu yetu.”

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, Matiko Chacha, alisema baada ya wanafunzi kusoma tangazo hilo waliamua kufanya maandamano mpaka ofisi ya serikali ya wanafunzi ili kupata uhakika kama wana taarifa na tangazo hilo na kwanini hawajashirikishwa.

“Sisi kama serikali ya wanafunzi tulikuwa hatuna taarifa juu ya uwapo wa tangazo hilo. Hivyo, tulishtushwa na ujio wao na tuliwajibu kuwa hakuna kitu kama hicho hata kama lilikuwa labda ni agizo kutoka utawala lazima lingepita katika ofisi zetu,” alisema Chacha.

Wanafunzi hao walimwonyesha kiongozi huo nakala ya tangazo hilo, ambalo halikuwa na  jina wala sahihi ya mwandishi.

Chacha alisema aliwatuliza wanafunzi hao na kufikia mwafaka baada ya kulichana tangazo hilo mbele yao na kuwahakikishia kutokuwapo kwa suala hilo na kwamba, hata kama lingekuwa ni la kweli, lazima lingepelekwa katika bunge la wanafunzi ili kufanyiwa maamuzi.

“Hata kama ikifikia hatua hiyo, lazima jambo hili lipitie  katika bunge la wanafunzi lenye wawakilishi kutoka kila darasa na kila kitivo ili kulifanyia uamuzi. Na pindi bunge likiridhia basi kutakuwa hakuna mjadala tena kutoka kwa wanafunzi kwani hao ndio wawakilishi wao,” alisema Chacha.

Alisema ni vigumu kwa wanafunzi wa chuo hicho kuvaa nguo fupi kutokana na uhalisia wa masomo yaliyopo kumtengeneza mwanafunzi kuvaa mavazi ya staha, kama vile suruali.

“Asilimia 90 ni masomo ya uchoraji. Masomo haya yanategemea meza maalumu. Na muda mwingi hutumia kwa kuinama. Pia hata mazoezi yake hufanyika vijijini sehemu, ambazo lazima watavaa mavazi ya kuwazuia na hatari ya kuchomwa na miba au kupata mikwaruzo,” alisema Chacha.

Afisa Utawala wa Chuo hicho, Syprian Majembe, alisema hajapata taarifa yoyote na kwamba, uongozi wa chuo haufahamu wala kuhusika na kitu hicho.

CHANZO: NIPASHE

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top