Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

DALADALA YATEKETEA KWA MOTO

Daladala likizimwa moto na kikosi cha moto Iringa 

Daladala yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ikiwaka moto eneo la mshindo.

Na: Denis Mlowe - Iringa Via Iringa Yetu.
 
Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayofanya shughuli za kusafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.
Ajali hiyo iliyotokea mida ya saa saba mchana ilihusisha daladala aina ya kipanya yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ilitokea katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo mkoani hapa.
Shuhuda ya ajali hiyo Anthony Zamilinga amesema kwamba gari hiyo ilikuwa ikitokea maeneo ya Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa. 
Msemaji wa Zimamoto Kaimu Mkuu wa Kituo Sajenti Meja John Zakaria amesema chanzo cha ajali hiyo hitalafu ya umeme iliyotokea katika gari hiyo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na tabia ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao. “kikosi cha zimamoto kinatoa elimu kila mara kuhusu elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kuna namba za simu za dharura ambazo ziko wazi wakati wote lakini wananchi hawana tabia ya kutoa taarifa mapema na ndio maana hasara kama hizi zinajitokeza hivyo hatuwezi kuota kama kuna janga la moto hivyo naomba ushirikiano wa wananchi katika majanga ya moto kama haya” alisema Sajenti Meja Zakaria
Mmiliki wa dala dala hiyo Ayubu Kabigi amesema kwamba amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo na amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari yake kwani wakati anapigiwa simu alikuwa anajiandaa na safari ya nje ya mkoa. “nawashukuru sana wananchi wa maeneo ya mshindo na kikosi cha zimamoto kuwahi kufika mara baada ya kupewa habari kuhusu janga hilo licha ya kwamba gari lilikuwa limewaka moto na kuteketea” alisema Kabigi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top