Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SIMBA YALIPA KISASI YANGA


Simba wakiomba dua kwa pamoja siku za hivi karibuni
MICHAEL MOMBURI
MKWARA wa Yanga kutaka kumsajili Mrisho Ngassa, umeishitua Simba ambayo imekimbia haraka kwenye ofisi za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na kukabidhi mkataba mpya waliosaini na winga huyo.

Simba inamtumia Ngassa kwa mkopo kutoka Azam FC ambayo ina mkataba naye hadi Mei 13 mwakani, lakini wiki mbili zilizopita viongozi wa Kamati ya Usajili ya walionekana na mchezaji huyo jijini Dar es Salaam na jana Jumatatu mmoja wao akaitamkia Mwanaspoti kwamba watamsajili kijana huyo msimu ujao.

Ngassa alipata dili la kwenda El Merreikh ya Sudan lakini akagoma kwenda huku Yanga ikidaiwa kuhusika kumshawishi kwa maelezo kwamba itampa dau kubwa baada ya kumaliza mkopo wake Simba.

Lakini Simba ambayo chini ya Katibu Mkuu, Evodius Mtawala, imeshamsainisha mkataba wa mwaka mmoja unaoanza Mei 31 mwakani, imeuwasilisha mkataba huo rasmi wiki iliyopita kwenye ofisi za TFF wakitaka uendelee pale ule wa Azam utakapokoma.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ndani ya Simba ni kwamba mkataba huo uliwasilishwa mapema ili kuondoa utata unaoweza kujitokeza baadaye.

"Tumewasilisha na tukawaambia kwamba uendelee pale huu wa Azam unapoishia kwa vile tayari Ngassa ni mchezaji huru, mkataba wake na timu iliyotuazima uko chini ya miezi sita," kilisema chanzo cha habari kutoka Simba.

Lakini kiongozi wa kamati moja nyeti ya TFF aliidokeza Mwanaspoti kwamba kitendo cha Simba kuwasilisha mkataba wa Ngassa kinaweza kuwagharimu kwani ni kinyume na kanuni.

"Ingawa Ngassa anaruhusiwa kuzungumza na klabu lakini haiwezi kumsainisha kwa wakati huu tena ikawasilisha TFF kwa ajili ya kusajili, ni kinyume na taratibu tena unaweza kuzuiwa kusajiliwa," alisema.

"Kama Azam ndiyo walitaka kuongeza mkataba sawa lakini si klabu mpya. Kama klabu inamtaka inabidi iwasilishe huu wa sasa wa Azam ukishakwisha.

Mmoja wa viongozi wa kamati ya usajili wa Yanga alidai jana kuwa: "Sisi tunajua tunachokifanya na tunajua tulichoafikiana, we subiri muda ukifika utaona kama atacheza huko Simba au Yanga.

"Lakini tunamtaka na kuna mambo inawezekana yameshafanyika, hatuwezi kuzungumza kwa undani tunaheshimu mkataba wake na Azam, huo mkataba wa Simba hatuujui."

Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza Januari 19 mwakani na ligi itamalizika Mei.

Ngassa amekuwa miongoni mwa wachezaji walioko kwenye fomu kwa sasa ingawa aliwaboa El Merreikh baada ya kugoma kwenda kuwachezea kwenye Ligi Kuu ya Sudan na michuano ya Afrika.HABARI KWA HISANI KUBWA YA MWANASPOTI
  
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top