Baada ya mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei kumtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho,
Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya
kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa
sasa.SOMA:MTEI AMTAKA ZITTO KABWE ASIGOMBEE URAIS 2015
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amefunguka baada ya watu wengi kumpigia simu na kumtumia ujumbe ili wapate kauli yake na yeye bila hiyana amefunguka na kuweka wazi kuwa mwaka 2013 hataongelea suala la urais 2015 hadi pale Katiba mpya itakapopatikana na pale chama chake kitakapoweka utaratibu wa namna ya kumpata mgombea Urais 2015.
Hapa chini ndivyo alivyoandika...
Ngoja
niweke wazi kabisa. Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya
kauli za wanachama waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala
hilo. Jibu langu kwa wote wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba
'katika moja ya maazimio yangu ya mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa
suala la Urais 2015. Hivyo sitaongelea suala hili. Sitasema kitu kuhusu
suala hili mpaka baada ya Katiba mpya kupatikana na chama changu kuweka
utaratibu na mchakato wake'.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Siasa
on Thursday, January 3, 2013
Post a Comment