Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HATIMAYE LULU AINGIA URAIANI

Elizabeth Michael (Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana jana asubuhi.
(picha: Raha za Pwani blog)

Elizabeth Michael (Lulu) Aachiwa Kwa Dhamana Leo Baada Ya Jana Kushindikana Kwa Sababu Msajili Wa Mahakama Alipata Udhuru, Leo Hii Msajili Alikuwepo Na Kudhibitisha Masharti Ya Dhamana Ya Lulu.
Hiyo ni baada ya jana kupata dhamana[SOMA:LULU APATA DHAMANA]  lakini akshindwa kutoka kwa sababu Msajili wa Mahakama hakuwepo[SOMA;LULU HAJAACHIWA

Kwa mujibu wa moja ya mawakili waliokuwa wanamuwakilisha mwigizaji huyu, Bwana Peter Kibatala, Siku ya leo, mambo yote yamefanikiwa kukamilishwa na hatimaye mwigizaji huyu ameweza kutoka Segerea na kuingia Uraiani leo hii.
Jaji Zanab Mruke amempatia Lulu dhamana hiyo chini ya kifungu namba 148 kifungu kidogo namba 1 na 2 cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2002.

Miongoni mwa masharti ya dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali na kila mmoja awe na fedha kiasi cha shilingi milioni 20, asitoke nje ya Dar es Salaam bila taarifa pamoja na kukabidhi hati zote muhimu zinazomhusu.

Lulu ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuua bila ya kukusudia alikamatwa tangu Aprili mwaka jana kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba huko Sinza Jijini Dar es Salaam.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top