Wachezaj wa Young Africans wakifanya mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Emmen FC ya Uholanzi
Timu ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza
mchezo wake wa mwisho na watatu (3) dhidi ya timu ya Emmen FC ya ligi
daraja la kwanza nchini Uholanzi katika mchezo wa kirafiki
utakaofanyika katika viwanja vya Adora football - Berek pembeni kidogo
ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeshakaa takribani siku 12
katika mji wa Antalya na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya
timu za Armini Bielefeld ya Ujerumani na Denizlispor ya Uturuki leo
asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence football
mjini Antalya.
Kocha Mkuu wa Young Africans
Ernest Brandts amesema atatumia mchezo huo wa mwisho kama fursa pekee
kwao kwani mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwao kwani timu ya Emmen FC
ni timu nzuri na ndio maana ipo katika ligi daraja la kwanza nchini
Uholanzi.
Akiongelea mchezo huo wa kesho Brandts
amesema timu ya Emmen FC ni timu nzuri, imekuja Antalya kuweka kambi ya
mafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi,
hivyo ni nafasi nzuri ya kujipima uwezo na timu hiyo ya Uholanzi.
Aidha
wachezaji Frank Domayo na Kelvin Yondani waliokuwa wameondoka jana
jioni kuelekea nchini Ethiopia wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao
wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya jana jioni kufika
Istambul kukuta tiketi zao za kwenda Addis Ababa ni za tarehe 09
Februari 2013 hali iliyopelekea kukwama Istambul na kuamua kurejea
mjini Antalya kuungana na wachezaji wenzao waliopo kambi.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo kambi mjini Antalya kimeendelea na mazoezi ya
asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa kesho amabao utakua ni mchezo wa
mwisho kabla ya timu ya Young Africans kuanza safari ya kurejea nchini
Tanzania siku ya jumapili.
Young Africans
inatarajia kuondoka mjini Antalya siku ya jumapili mchana kupitia
Istambul ambapo itaondoka majira ya saa 1 usiku, saa 2 usiku kwa saa za
Afrika Mashariki na inatarajiwa kufika Dar es salaam Tanzania majira ya
saa 10 usiku kasoro.
Jerson Tegete, Omega Seme & Ladislaus Mobgo wakiwa mazoezini leo asubuhi
CHANZO:YANGA


Post a Comment