Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Denizlispor fc katika
mchezo wa kirafiki uliofanyika leo katika viwanja vya Selen Football -
Kalemya Complex
Young Africans imepoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya
timu ya Denizlispor FC ya Uturuki kwa mabao 2-1 katika mchezo
uliofanyika katika viwanja vya Selen football - Kamelya Complex pemebni
kidogo ya mji wa Antalya.
Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la
mapema zaidi lakini umaliziaji wa washambuliaji Saimon Msuva na Jerson
Tegete katika dakika za 7, 15 na 24 uliikosesha mabao ya mapema.
Young
Africans ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35,
mfungaji akiwa ni Jerson Tegete akimalizia pasi safi iliyopigwa na
Saimon Msuva kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Athuman Idd
'Chuji'
Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi
chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans
ilikuwa mbele kwa bao 1-0
Kipindi cha pili Denizlispor FC ilifanya
mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji
wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa
walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma
Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'
Dakika
ya 78 Denizlispor FC ilijipatia bao lake la kwanza, baada ya mfungaji
kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni ili hali walinzi wa
Young Africans na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' wakisubiri
kusikia filimbi ya mamuzi kwani mfungaji kabla ya kufunga alikuwa
ameunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Huku mpira ukiwa katika
dakika za mwisho kabla ya kumalizika, mwamuzi wa mchezo ambaye
hakuonekana kuwa makini aliwapatia wenyeji Denizlispor FC penati dakika
ya 88, penati ambayo ilileta utata kutokana na mwamuzi kupishana na
mshika kibendera aliyekuwa ameonyesha kuwa mshabuliaji wa Denizlispor
alikuwa amemfanyia madhambi nahodha Nadir Haroub, Denizlispor FC
walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 2 Denizlispor FC.
Wachezaji wa Young Africans wakisalimiana na wachezaji wa Denizlispor kabla ya kuanza kwa mchezo leo jioni
,,,,,,,,,,,,,,,,
Kocha mkuu Ernest Brandts hajapendezewa na matokeo hayo na hasa
akitupa lawama zake kwa mwamuzi amabaye alishindwa kulimudu pamabano
hilo ambapo katika kipindi cha pili alitoa maamuzi ya utatanishi
yaliyopelekea timu yake kupoteza mchezo huo.
Timu yangu imecheza
vizuri, nadhani wote tulikuwa mashuhuda jinsi vijana walivyocheza soka
safi la kuvutia lililowashangaza baadhi ya wapenzi wa soka waliokuwa
wamefika kutazama mchezo huo, naamini timu yangu kwa sasa iko vizuri na
wachezaji wanaonekena kuelewa vizuri mafundisho yangu alisema 'Brandts'
Young Africans kesho itaendelea na mazoezi asubuhi katika viwanja vya Hoteli ya Fame Residence football .
Young Africans:
Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, Kabange Twite, Nadir Haroub
'Cannavaro', Kelvin Yondani/Mbuyu Twite, Athumani Idd 'Chuji, Saimon
Msuva/Oscar Joshua, Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu,Jerson
Tegete/Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima
CHANZO:YANGA


Post a Comment