Collins Mbesuma wa Zambia akipiga shuti lililompita Kipa Zerihun Tadellewa Ethiopia na kuiandikia goli Zambi.(Picha na Daily Mail)
Mashabiki wa Ethiopia wakiwa wamejazana uwanjani hapo huku wakiwa na wamevaa jezi za timu ya Taifa na bendera hakika walikuwa kivutio uwanja wa Mbombela .Picha na (Daily Mail)
Kipa wa Zambia Kennedy Mweene akiruka na kuokoa shuti la penati kutoka mchezaji wa Ethiopia Saladin Said.(Picha na Daily Mail)
Adane Girma akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake ya Ethiopia katika mchezo wao na Zambia mechi iliyoisha kwa kutoshana nguvu ya bao 1-1.(Picha na Daily Mail)
...........
Mabingwa watatezi wa kombe la mataifa ya Afrika
Chipolopolo ya Zambia wameanza kampeini ya kutetea kombe hilo
waliloshinda mwaka uliopita kwa kutoka sare ya kufungana bao moja kwa
moja na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya Kundi C nchini Afrika Kusini.
Kinyume na matarajio ya wengi Ethiopia
ilionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo na mara nyingi wachezaji
wake wakionekana kuwathibiti wachezaji wa Chipolopolo.
Kwa mara nyingine tena timu hiyo ya Zambia, imeonyesha kuwa kwa sasa haiko katika hali nzuri kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Wakati wa mechi hiyo beki wake Chisamba Lungu
alimuangusha mshambulizi wa Ethiopia Saladin Seid, kwenye eneo la hatari
na bila kusita refa wa mechi hiyo akatoa adhabu ya penalti.
Lakini kipa wa Zambia Kennedy Mweene aliokoa mkwaju uliopigwa na Seid na hivyoi kufufua matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Dakika chache baadaye, kipa wa Ethiopia, Jemal Tassew alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Chisamba Lungu.
Licha ya kuwa alikuwa akiondolewa uwanjani kwa
machela refa wa mechi hiyo alimpa kipa huyo kadi nyekundu kutokana na
mchezo mbaya na hatari aliouonyesha.
Dakika chache baada ya tukio hilo mabingwa hao
watetezi wakafunga bao lao la kwanza kupitia kwa mchezaji Collins
Mbesuma kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili licha ya kucheza
wachezaji kumi pekee kwa muda mrefu, Ethiopia ilisawazisha kunako dakika
ya 65 kupitia kwa mchezaji Adane Girma.
Ithiopia ilithibiti mpira wa asilimia kubwa katika kipindi cha pili na hivyo kuzima matumaini ya mabingwa hao watatezi.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Mechi itakayofuatia itakuwa kati ya Nigeria na Burkina Faso
HABARI NA BBC Swahili




Post a Comment