Kwa ufupi
Habari za uhakika toka ndani ya wajumbe wa kikao
hicho, zimeeleza kuwa kikao hicho, ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, kilifikia uamuzi wa kurejewa
uchaguzi huo, baada ya kuridhika kuwa Laizer hakupata nusu ya kura
katika uchaguzi huo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Arusha, imependekeza kurejewa uchaguzi wa nafasi
ya mjumbe wa Halmashauri Kuu(Nec) kutoka Wilaya ya Longido nafasi
ambayo awali Mbunge wa jimbo hilo, Lekule Laizer alitangazwa kushinda.
Habari za uhakika toka ndani ya wajumbe wa kikao
hicho, zimeeleza kuwa kikao hicho, ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, kilifikia uamuzi wa kurejewa
uchaguzi huo, baada ya kuridhika kuwa Laizer hakupata nusu ya kura
katika uchaguzi huo.
Mjumbe mmoja wa kamati hiyo, alisema katika
uchaguzi huo wa Nec mwaka mwa jana, uliofanyika mwishoni mwaka jana,na
kusimamiwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Arusha, George Kijazi
Laizer alipata kura 417,Peter Lemshau kura 381 na Michael Sakino kura
58.
“Katika uchaguzi huo, kura halali zilikuwa ni 871
na kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, hapa hakupatikana mshindi na
Laizer na Lemshau wanapaswa kurudia uchaguzi lakini cha ajabu Laizer
alitangazwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwa ni
mjumbe wa NEC”alisema mjumbe huyo.
Mjumbe huyo alisema mapendekezo hayo, tayari
yamepelekwa sekretarieti ya CCM taifa na yanatarajiwa kutolewa uamuzi na
kamati kuu ambayo inatarajiwa kupatikana mwishoni mwa wiki hii.
Hata hivyo, wakati kamati ya siasa mkoa
ikipendekeza kurejewa kwa uchaguzi huo, tayari kuna uvumi kuwa, Laizer
huenda akateuliwa kugombea nafasi ya kamati kuu ya CCM hasa kutokana na
kuungwa mkono na vigogo kadhaa wa chama hicho.
“Tumepata taarifa kuwa atateuliwa kugombea kamati
kuu,sasa hili litakuwa ni jambo la ajabu kwani bado hajawa mjumbe wa NEC
kwa nini ateuliwe kuwa mjumbe wa kamati kuu”alihoji kiongozi huyo.
Kwa upande wake, Lemshau alipotakiwa kuelezea
hatma yake alisema anasubiri maamuzi ya ngazi za juu kwani tayari
alipeleka vielelezo vyake.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Arusha, Issack
Joseph alipotakiwa kuelezea maamuzi ya kamati ya Siasa ya mkoa kuhusiana
na kurejewa kwa uchaguzi huo wa NEC Longido ,alisema kikao cha kamati
kuu ni cha siri,hivyo lakini hata hivyo hakukanusha wala kukubali kama
walipendekeza kurejewa uchaguzi huo.
NA MWANANCHI
NA MWANANCHI
Post a Comment