Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CCM WAJIBU MAPIGO YA CHADEMA

Juliana Shonza akihutubia wakazi wa Temeke juu ya maamuzi yake thabiti ya kujiunga na CCM

Mtela Mwampamba akiwaeleza wananchi wa Temeke mapungufu makubwa ya kidemokrasia yaliyopo kwenye vyama vya upinzani na hivyo kumfanya yeye binafsi kuchukua uamuzi wa kujiunga na CCM.

Saumu Kisena akionyesha kitambulisho chake , Saumu amejiunga rasmi CCM baada ya kugundua chama alichokuwepo kinahubiri haki nje wakati ndani hamna haki kabisa.

Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi, akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Ndugu Sophia Mjema akiwapungia wananchi wa Temeke wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile ,Temeke ,Mwisho.

Wananchi na Wapenzi wa CCM kutoka kata ya Kilakala,Yombo kama walivyojitambulisha ,walisema Nape ameongea mambo mengi ya msingi na kumtakia heri aendelee kufanya kazi nzuri.

Wasanii wa kikundi cha TMK wakitoa burudani kwenye uwanja wa nyumbani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke,tarehe 16/2/2013.

Baadhi ya wananchi wakionekana kuelewa vizuri maneno ya viongozi wao.

Kikundi cha Hamasa cha CCM,Temeke kikihamasisha kwa aina yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile,Temeke.

 GAZETI LA MWANANCHI NALO Limeandika...
WIKI moja baada ya Chadema kufanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam na kuwashukia Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, CCM jana ilifanya mkutano katika viwanja hivyo, huku ikijibu hoja zilizotolewa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Mkutano huo wa Chadema ulifanyika Jumapili iliyopita, ambapo viongozi wake walitoa tuhuma mbalimbali kueleza jinsi Spika Makinda na naibu wake walivyotupa hoja za Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na James Mbatia ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe alisema hoja ya Mnyika kuhusu uhaba wa maji katika Jiji la Dar es Salaam, ilitupwa kwa kuwa alichokuwa akikizungumza mbunge huyo, kilikuwa kikifanyiwa kazi na Serikali.
“Mnyika anatakiwa kutosherehekea mimba wakati mwenye mtoto ni CCM, Serikali ya CCM ndiyo imeweka miradi iliyopo katika Jimbo la Ubungo na inaiendeleza,” alisema Maghembe.
Alifafanua kwamba Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini utakamilika kujengwa mwishoni mwa mwezi huu na utazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.
“Serikali imejianda kuhakikisha kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unakuwa na maji ya kutosha katika mpango wake wa muda mfupi na mrefu. Katika mpango wa muda mfupi mpaka kufikia Aprili 2014, maji yatakuwa ya kutosha katika jiji hili,” alisema Maghembe.
Alisema kuwa hivi sasa Serikali ipo katika mpango wa kutandaza mabomba ya maji kutoka Ruvu Juu kwenda Dar es Salaam kupitia Bagamoyo, ambapo utaenda sambamba na uchimbaji wa visima 84.
Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Neema Himid alisema kuwa hoja iliyowasilishwa na Mnyika bungeni ilikuwa ni; ‘Copy and Paste’, (ya kamati hiyo).
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.

 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top