Mwenyekiti wa Simba ismail Aden Rage (Picha na Maktaba yetu)
Baada ya Klabu ya Simba kukubali kipigo cha goli moja kutoka kwa wakata miwa wa manungu Mtibwa Sugar sasa presha imemuelemea Mwenyekiti wa Simba Aden Rage kuachia ngazi klabuni hapo.
Wapenzi na wanachama wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi wenye kuvaa jezi rangi nyekundu na nyeupe wamesikika wakitoa wito kwa mwenyekiti wao luachia ngazi mara moja.Je Mwenyekiti Rage ana lipi la kusema kuhusiana na matokeo mabovu ya Klabu yake ? Tusubiri tuone pale atakapopatikana na kuongea na vyombo vya habari.
Post a Comment