Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwa ufupi
Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa
na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo
zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita
katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera,
uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi
ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya
mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama
hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba
jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa
huo kupitia CUF.
Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo
uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya
uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho
kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera,
uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi
ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.
Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara
baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na
viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya
mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la
kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya
kwenda kuhutubia.
Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba
alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi
za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi
umasikini ni kumpatia fedha taslimu.
Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya
uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia
teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa
vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.
Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2
imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali
ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa
na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake
kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali
zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya
utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu
wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.
NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria. Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka.
NA MWANANCHI

Post a Comment