Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LISSU,DK.KIGWANGALA WAPIMANA UBAVU BUNGENI

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, jana alilazimika kuingilia kati malumbano kati ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala (CCM).
Lissu na Dk. Kigwangala walilumbana jana wakati Dk. Kigwangala alipokuwa akihitimisha hoja yake kuhusu kuanzishwa mfuko wa mikopo ya vijana wanaotaka kuwekeza katika kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo.

Wakati akihitimisha hoja hiyo, Dk. Kigwangala alimshutumu Lissu kwa kukataa hoja yake bila kujali umuhimu wa kuwepo kwa mikopo ya kuwawezesha vijana kujiajiri kwamba mpango huo ni muhimu kwa ustawi wa jmii.

“Mheshimiwa nakushukuru sana, nakumbuka mwaka 2006 ulikuwa mgonjwa wangu kwa sababu nilikutibu.”

Wakati Dk. Kigwangala akiendelea kuchangia, Lissu alilazimika kuingilia kati kwa kuomba utaratibu, akitumia kanuni ya 68 sehemu ya kwanza pamoja na ile ya 63 sehemu ya kwanza zinazokataza mbunge kusema uongo bungeni.

“Mheshimiwa Naibu Spika, mimi sijawahi kuwa mgonjwa wa Mheshimiwa Kigwangala, mwaka 2006 anaosema, yeye na madaktari wenzake walikuwa wamefukuzwa kazi, mimi kwa taaluma yangu nikaenda kuwatetea bure mahakamani wakarudishwa kazini.

“Kwa maana hiyo, naomba asiseme kwamba mimi niliwahi kuwa mgonjwa wake, hilo silikubali,” alisema Lissu.

Kutokana na kauli hiyo ya Lissu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliingilia kati na kumtaka Dk. Kigwangala afute kauli yake na kuhitimisha hoja yake.

Baada ya mjadala huo kuonekana kupoteza mwelekeo, Jaji Werema alisimama na kumtaka Dk. Kigwangala afute kauli yake dhidi ya Lissu kisha akamtaka awe makini na kauli zake.

Dk. Kigwangala alikubali kufuta kauli hiyo na hoja kuhitimishwa, huku ikiungwa mkono na wabunge wengi.

NA MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top