Wachezaji wa Mali wakifurahia baada ya kukabidhiwa medali zao za ushindi wa tatu baada ya kuidungua Ghna kwa goli 3-1.
(Picha na Daily Mail)
Mali yatwaa nafasi ya tatu katika michuano ya Fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2013 zinazokamilika kesho,
Jumapili nchini Afrika Kusini.
Mali ilipata goli la kuongoza katika kipindi cha
kwanza katika dakika ya 21 likifungwa na Mahamadou. Hadi mapumziko Mali
ilikuwa ikiongoza kwa hilo goli.
Mahamadou Samassa akishangilia baada ya kuifungia Mali goli la kwanza mjini Port Elizabeth.(Picha na Daily Mail)
Kipindi cha pili kilianza kwa Mali tena kufunga katika dakika ya 48, mfungaji akiwa ni Seydou Keita.
Seydou Keita akicangalia kwa makini mpira ukiingia nyavuni huku golikipa wa Ghana akiwa hana la kufanya katika mechi y kutafuta mshindi wa tatu.Mechi iliisha kwa Mali 3-1 Ghana(Picha na Daily Mail)
Ghana ilijitutumua na kupata bao la kufutia
machozi katika kipindi hicho cha pili. Hata hivyo furaha yao haikudumu
sana baada ya kuchapwa goli lingine la tatu na la ushindi kwa Mali.
Matokeo haya yanaendeleza ubabe wa Mali dhidi ya
Ghana, ambapo mwaka jana katika mchezo kama huo wa kutafuta mshindi wa
tatu wa michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2012, Mali
iliichapa Ghana 2-0.
Ni mwaka mmoja kamili, wakati Ghana na Mali
zilipokuwa zikijiandaa kucheza mechi ya kusaka nafasi ya tatu baada ya
timu zote mbili kupoteza matumaini ya ubingwa zilipotolewa katika nusu
fainali za michuano ya kombe la Afrika za mwaka 2012.
Mchezo huu, unatoa fursa ya kuhitimisha michuano
hiyo ambapo bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2013
atapatikana, ukizikutanisha Nigeria na Burkina Faso hapo keho.
Ghana na Mali baada ya kukosa kombe hili,
jitihada zinaelekezwa katika kutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe
la dunia za mwaka 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.
HABARI NA BBC SWAHILI
Post a Comment