Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini,
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili
kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata
ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua
na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.
Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho
cha Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini leo
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama
Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya
CCM ya Kata hiyo leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi
ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi
(kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje mkoani Lindi leo
Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama
vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama
Salma Kikwete leo
Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa
Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo
Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi
Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo
Ilikuwa aisye na mwana aelekee jiwe: mama akiwa na watoto wake kwenye mkutano huo. (picha zote na Bashir Nkoromo).
Post a Comment