TUNDA
 la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa 
karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo 
vya afya, utafiti umebaini.
 
Utafiti 
huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, 
umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya 
matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu 
ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani 
pasipo kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine 
za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa 
kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani, 
mwaka 2010.
Taasisi ya  utafiti  wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya  utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika 
utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina 
uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa 
kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa
 kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia  jina la kibiashara
 la ‘Triamazon’  na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na 
Marekani  kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.
Utafiti 
mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na 
kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia  ulibaini kuwa stafeli lina 
uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti 
wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga 
seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo 
tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la 
Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho 
ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani.
Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na
 kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia 
huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya 
mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti  
huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo kinaweza  
kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na 
madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na 
kunyonyoka nywele.
CHANZO: http://thedonsimon.blogspot.com/
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment