Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CCM NAYO YACHUNGUZA MATOKEO KIDATO CHA IV


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Abdallah Bulembo
Wakati serikali ikiwa imeunda Tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka jana, Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nayo imeunda kamati maalumu kuchunguza anguko la elimu nchini.

Jumuiya hiyo inayomiliki shule za sekondari 72, ni moja ya taasisi zilizopata pigo kubwa kutokana na matokeo hayo mabaya.


Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo, alisema wao kama wazazi, matokeo hayo yamewakwaza sana na hasa ikizingatiwa pia kuwa ni wadau wa elimu nchini.


“Tulikuwa na kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Jumuiya yetu, jambo kubwa lililotawala kwenye kikao hicho ni kuhusu anguko la elimu ya sekondari.

“Sisi kama wadau wa elimu, tumelazimika kuunda kamati kutafuta sababu za anguko hilo, kamati hiyo itatoa matokeo yake kwenye kongamano la elimu litakalo fanyika Aprili tano mjini Tanga ambako wadau watajadili mambo mbalimbali,” alisema.

Kwa mujibu wa Bulembo, baada ya majibu ya kamati hiyo, mbali na kujadiliwa kwenye kongamano hilo, pia ushauri utapelekwa serikalini kabla ya Tume iliyoundwa na  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, haijatoa majibu yake.


Alisema kuwa pamoja na matokeo mabaya, lakini baadhi ya shule za jumuiya hiyo zilifanya vizuri.


Bulembo alisema matokeo ya 2011 yalikuwa ni mazuri ikilinganishwa na ya mwaka jana kwa shule za jumuiya hiyo.


Alitoa mfano kuwa mwaka 2011 daraja la kwanza walikuwa 21, la pili 112, la tatu I401, la nne  655 na sifuri 2063.


Kwa mwaka jana ufaulu kwa shule hizo alisema daraja la kwanza walikuwa 9, la pili 77, la tatu 263, la nne 2,499 na sifuri  zaidi ya 3,000. Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi alisema Kamati ya kuchunguza anguko hilo itaongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia Wazazi, Jackson Rweikiza.

 
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top