KWA wiki kadhaa mfululizo nimekuwa nikikuletea makala za matunda na miti inayotumika kutibu magonjwa mbalimbali.
Makala ya leo itaangazia magonjwa yanayowatesa Watanzania na kushindwa kujua namna ya kupona, huku wengine wakihusisha na imani za kishirikina.
Miongoni mwa magonjwa hayo ni vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye kuta za njia ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Dk. Mohamed Mkweli kutoka Kliniki ya Herbal anasema vidonda vya tumbo huwaathiri zaidi watu wenye umri kati ya miaka 40 hadi 60.
Anasema wanawake wanapofikia umri wa kutopata hedhi na watu wenye damu kundi O hupata vidonda vya tumbo zaidi kuliko wenye damu makundi mengine.
Chanzo
Dk. Mkweli anasema chanzo ni kushambuliwa na bakteria waitwao Helicobacter pylori ambao wakiingia mwilini hushambulia kuta za tumbo na kuondoa ngozi inayoziba juu na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
“Kuzalishwa kwa wingi kwa hydrochloric acid (HCL), na hivyo acid hii humeng’enya kuta za tumbo, lakini pia wasiwasi, ikiwa mtu ana msongo wa mawazo itaathiri hamu ya kula na hivyo enzymes hazitakuwa na chakula cha kumeng’enya na badala yake zitameng’enya kuta za tumbo,” anasema.
Vyanzo vingine anasema ni uywaji wa pombe, uvutaji sigara, unywaji wa vinywaji vyenye caffeine, matumizi ya dawa za kuondoa maumivu kama vile aspirin na ibuprofen.
Dk. Mkweli anasema kuna aina mbili za vidonda vya tumbo ambazo ni vidonda vilivyoko tumboni ambavyo dalili zake kuu ni kuhisi maumivu hasa baada ya kula chakula.
Aina ya pili ni vidonda vilivyoko kwenye utumbo mwembamba na dalili zake ni kuhisi maumivu hasa kabla ya kula.
Moyo kutanuka
Dk. Mkweli anasema ugonjwa huu unaufanya moyo kuwa dhaifu na kushindwa kusukuma damu vizuri kuelekea sehemu mbalimbali za mwili.
Anasema tatizo hilo huwapata sana wanaume kuliko wanawake, pia huwapata wenye umri kati ya miaka 20 hadi 60 na watoto wadogo.
Sababu
Dk. Mkweli anaeleza kuwa misuli ya moyo hutanuka kutokana na kushambuliwa na sumu zilizomo mwilini.
Sumu hizo hushambulia seli zinazounda misuli ya moyo na hivyo kuifanya iwe dhaifu na kushindwa kusukuma damu mwilini.
“Sababu nyingine ni unywaji wa pombe, magojwa ya tezi, shinikizo la juu la damu. Kinamama wajawazito pia hupata tatizo hili la moyo kutanuka, lakini mara nyingi huisha pindi wanapojifungua,” anaeleza.
Figo
Figo ni kiungo muhimu mwilini ambacho hufanya kazi za kuchuja taka zilizoko kwenye damu, kuchukua baadhi ya vitu vinavyohitajika mwilini na kurudisha kwenye mzunguko wa damu.
Dk. Mkweli anasema kuwa figo huchuja lita 180 kwa siku lakini ni lita 1.5 hadi 2 ndio hutolewa kama mkojo kwa siku kwa mtu mzima asiye na tatizo la kiafya.
Dk. Mkweli anasema kuwa ugonjwa huu, figo hushindwa kufanya kazi zake kwa muda fulani lakini hutibika.
Anaeleza kuwa dalili zake ni kupungua kwa kiwango cha mkojo na kufikia chini ya 400ml kwa siku kwa mtu mzima na chini ya 0.5ml kwa watoto.
Anasema mara nyingi ugonjwa huu huanza taratibu na huonesha dalili chache, lakini baada ya muda tatizo huwa sugu na kuleta madhara makubwa.
Dk. Mkweli anasema kuwa figo inaposhindwa kuondoa maji mwilini itasababisha miguu, mikono, uso kuvimba, kushindwa kupumua vizuri na maji kujaa kwenye mapafu, kupoteza hamu ya kula, kushindwa kupata usingizi na ngozi kuwa nyeusi.
Mgandamizo wa juu wa damu
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa ya arteries, na hivyo kuufanya moyo ufanye kazi zaidi ili uweze kusukuma damu.
“Kwa kawaida msukumo wa damu hutegemea wakati misuli ya maumivu ya kichwa hasa sehemu ya nyuma ya kichwa kupoteza uwezo wa macho kuona, kupoteza fahamu,” anasema Dk. Mkweli.
Anasema umri mkubwa husababisha misuli ya moyo kulegea na kushindwa kufanya kazi na matumizi ya vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
Anasema kwa kutumia tiba mbadala amefanikiwa kuwatibu baadhi ya watu waliokuwa wakisumbuliwa maradhi hayo.
Dk. Mkweli anasema cheti chake alichopewa na mkemia wa serikali pamoja na Wizara ya Afya baada ya kupeleka dawa zake katika uchunguzi imekuwa chachu ya kuaminika na kuponyesha wagonjwa mbalimbali.
“Magonjwa haya husababisha vifo vya ghafla, tatizo ndugu mwandishi wenye magonjwa makubwa kama hayo ndio wale wasioamini katika tiba mbadala na matumizi ya matunda na miti ambayo ipo hapa nchini.
“Wengi nilioanza kuwatibia walikuwa na hofu kuwa mimi ni tapeli, lakini baada ya kutumia dawa waliamini na sasa wanapona,” anasema.
Dk. Mkweli anatoa wito kwa Watanzania kupenda asili yao na kufanya mazoezi, kunywa maji kwa wingi na utumiaji wa matunda kabla hawajaugua.

HISANI YA Happiness Mnale 0713 477 725 mnaleh@yahoo.com VIA Tanzania Daima
Post a Comment