*Wamo wakuu wa upelelezi wa mikoa, FFU
*Wengine walificha dawa za kulevya
*Wengine walificha dawa za kulevya
SERIKALI
imewasimamisha kazi na kuwafungulia mashitaka ya kijeshi maofisa watano
wa Jeshi la Polisi kutokana na tuhuma mbalimbali za maadili na taratibu
za jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema maofisa hao
wamesimamishwa, baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kwa kila mmoja
kulingana na tuhuma zao.
Aliwataja maofisa hao, kuwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya, Elias Mwita na Msaidizi wake, Jacob Kiango, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya, Charles Kinyongo.
Alisema maofisa hao, walipatikana na kosa la kuficha dawa za kulevya, zilizokamatwa Machi 2012 katika kituo cha ukaguzi cha Tunduma na badala yake kuweka sukari na chumvi na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.
“Baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya uchunguzi, alibaini si dawa za kulevya, bali ni sukari na chumvi kitendo ambacho Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoani Mbeya, iliniandikia barua kutaka uchunguzi ufanyike upya.
“Niliamua kuunda tume nyingine ambayo ilibaini kilichokamatwa sio kilichowasilishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, hivyo nimeagiza waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria na tayari wamesimamishwa kazi tangu jana (juzi),” alisema.
Alisema ofisa wa nne, aliyesimamishwa kazi kutokana na kosa la kupiga wananchi na kuwabambikizia kesi za jinai zisizo na dhamana ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kagera, Peter Matangi.
Alisema chanzo cha ofisa huyo kuwapiga wananchi ni kutokana na mgogoro wa ardhi, uliotokea kati ya mwekezaji na wananchi wa Kata ya Nyakasimbi na kusababisha kuwapo na maandamano.
Alisema baada ya wananchi zaidi ya 14 kuingia katika eneo la shamba hilo, askari waliwakamata wananchi na kufunguliwa kesi za jinai zisizo na dhamana, ambapo walikaa gerezani miezi minne.
“Katika mgogoro wa ardhi, tuliunda tume ya kwanza ikafanya uchunguzi, lakini hakupata majibu mazuri ambapo nililazimika kuunda tume ya pili na mimi nikawa mwenyekiti ndipo tulibaini kumbe wananchi walibambikiwa kesi zisizo zao.
“Katika hili, tumeagizwa aliyehusika asimamishwe kazi na kufunguliwa mashitaka, hii ni mwanzo wa kutekeleza maazimio tuliyofikia hivi karibuni katika kikao cha maofisa wa Jeshi la Polisi mjini Dodoma, kulisafisha jeshi letu,” alisema.
Ofisa wa tano, aliyesimamishwa kazi kwa mwezi mmoja akisubiri baraka rasmi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na cheo chake kuwa Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ni Renatusi Chalamila.
Alisema ofisa huyo, alipatikana na kosa la kudai na kupokea fedha kama rushwa, ili kutoa ajira kwa vijana katika Jeshi la Polisi.
Alisema Chalamila, amekuwa akilalamikiwa sehemu nyingi kujihusisha na vitendo hivyo, ambapo tume ilibaini malalamiko hayo ni ya kweli.
“Huyu kutokana na cheo chake, Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kumfukuza kazi, hivyo tumempa likizo ya mwezi mmoja tukisubiri baraka za Rais na atafunguliwa mashitaka kwenye vyombo vya sheria,” alisema.
Alisema ofisa wa sita, ni Mrakibu wa Polisi kituo cha Mugumu, SSP Paul Mng’ong’o ambaye aliingia katika hifadhi ya Mbunga ya Serengeti na kupanga njama za kuchimba madini aina ya dhahabu ambaye pia atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Alisema maofisa wote, walisimamishwa kazi juzi na taratibu za kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria zitaandaliwa.
Pamoja na mambo mengine, alisema malalamiko ya wananchi yaliyokuwa yakitolewa dhidi ya jeshi la polisi kuwabambikizia kesi, limeonekana ni kweli ambapo aliahidi kuondoa kasoro hiyo.
Kuhusu suala la kutekwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd Absalom Kibanda, alisema hilo ni suala dogo ambalo hawezi kulizungumzia.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka waandishi wa habari, wamuulize Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kwa kuwa ndiye mwenye jukumu hilo.
Dk. Nchimbi alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua juu ya suala la kutekwa kwa Kibanda.
“Suala la Kibanda ni suala ambalo halipo katika ‘level’ (kiwango) cha waziri kulizungumzia.
“Muulizeni Kova, hilo ni suala lililo upande wake.
“Kama mkiona imeshindikana, basi mniambie tumpigie simu tujue anasemaje, hili ni suala ambalo lipo katika mambo ya kawaida ya kiupelelezi, siyo level yangu kuzungumzia,” alisema Dk Nchimbi.

NA MTANZANIA
Post a Comment