Ndugu zangu,

Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake haifai ikapita bila kujadili masuala ya msingi yenye kumhusu mwananmke na mahusiano yetu; wanawake na wanaume hususan kwenye kusaidiana malezi ya watoto wetu.

Kwa mwananme, mara nyingi jukumu la kumlea mtoto anamwachia mwanamke, haya ni mapungufu. Haitoshi tu kwa mwanamme kuacha hela ya chakula na mboga nyumbani. Kuna kufuatilia maendeleo ya watoto, ikiwamo shule.

Nitoe mfano, jana nikiwa hapa Morogoro kamanda wangu mmoja amenipigia simu akiwa nyumbani Iringa kuniomba nimsaidie na kazi yake ya shule kuhusu historia. Ananitegemea pia kuwa ni msaada kwake kwa mambo ya shule. Hivyo, ikanibidi niwaombe radhi wenzangu kuwa nisingekuwa nao baada ya saa kumi na mbili jioni kwa vile nahitajika nirudi nilipofikia na kuanza kazi niliyopewa na mwanangu. Kumsaidia kufafanua masuala ya historia. 

Hoja yangu hapa, ni kuwa wanaume, pamoja na majukumu yetu mengi, tuna wajibu wa kutenga muda nyumbani walau wa kuwauliza watoto wetu juu ya maendeleo yao ya shule. Kuyaangalia madaftari yao pia.
Na hapa mwanamme uanze kwa kujiuliza; Ni lini mara ya mwisho umeliangalia daftari la mtoto wako? Au ni kazi uliyomwachia mkeo tu?

Happy International Women Day!A
CHANZO:www.dewjiblog.com