Timu ya Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya
Mgambo Shooting ya mjini Tanga katika mchezo uliofanyika leo jioni
katika uwanja wa mkwakwani, mchezo ambao ulikosa radha kufuatia waaamuzi
wa mchezo huo kutoa maamuzi ya kutatanaisha muda wote wa mchezo.
Mgambo Shoooting ambayo imefikisha pointi 25 mara baada
ya mchezo wa leo, iliingia uwanjani kuhakikisha inapata pointi tatu ili
iweze kujinusuru katika janga la kushuka daraja hali iliyopelekea
kuuanza mchezo kwa kasi.
Young Africans ilifanya
mashambulizi langoni mwa Mgambo kupitia washambuliaji wake Hamis Kiiza,
Nizar Khalfani na Saimon Msuva ambapo waliweza kosa mabao ya wazi dakika
20 za mwanzo kufuatia kutokua makini katika umaliziaji.
Frank
Domayo alipiga shuti kali langoni mwa timu ya Mgambo ambapo mlinda
mlango wao aliukoa mchomo huo ambao ulitoka na kupigwa kona ambayo
haikuzaa matunda yoyote.
Dakika ya 35 Hamis Kiiza
alichelezewa ndivyo sivyo na mlinzi wa Mgambo Shooting lakini katika
hali isiyo ya kawaida mwamuzi alikaa kimya kuashiria kuwa hakuchezewa
madhambi, hali iliyopekea washabiki na wapenzi wa soka kumzomea mwamuzi.
Dakika
ya 42 ya mchezo, Mgambo Shooting walipata bao la kwanza kufuatia
walinzi wa Yanga kutokua makini na mfungaji kumalizia krosi iliyotoka
upande wa kushoto na kumfunga mlinda mlango Ally Mustafa.
Dakika
ya 44 Saimon Msuva alikwatuliwa ndani ya eneo la hatari hali
iliyopelekea mchezaji huyo kutolewa nje na machela lakini mwamuzi
aliendelea kupeta na kuonyesha kuwa Msuva kajidondosha ndani ya eneo
hilo.
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, Young Africans 0 - 1 Mgambo Shooting.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambapo iliwangiza Haruna
Niyonzima, Said Bahaunzi na Nurdin Bakari kuchukua nafasi za Hamis
Kiiza, Oscar Joshua na Frank Domayo mabadiliko ambayo yalileta uhai
zaidi eneo la kiungo.
Yanga
iliendelea kulishambulia lango la Mgambo kusaka bao la kusawazisha huku
Mgambo wakipoteza muda kwa kujidondosha mara kwa mara huku wakidhani
wataibuka na ushindi katika mchezo wa leo.
Dakika
ya 87 ya mchezo kiungo Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao la
kusawazisha kufuatia migongeo mizuri kati yake na David Luhende ambapo
Msuva alipiga shuti lililomgusa mlinzi wa Mgambo wakati akitaka kuokoa
mchomo huo ambao uliingia moja kwa moja na kuhesabu bao la kusawaisha.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Mgambo Shooting 1 - 1 Young Africans.
Kwa
matokeo hayo ya leo Young Africans inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi
Kuu ya Vodacom baada ya kufikisha pointi 53 ikiwa ni pointi 6 mbele ya
timu ya Azam inayokamata nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 47.
Kikosi
cha Young Africans: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar
Joshua/Haruna Niyonzima, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani,
6.Athumani Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Frandk Domayo/Nurdin Bakari,
9.Hamis Kiiza/Said Bahanuzi,10.Nizar Khalfani 11.David Luhende
Post a Comment