Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

OUT YATOA MAFUNZO KWA SADC

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimeanza kutoa mafunzo ya elimu huria na masafa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo jumla ya washiriki 40 kutoka nchi wanachama 15 wanashiriki mafunzo hayo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mkuu wa OUT, Profesa Tolly Mbwete, alisema mafunzo hayo yameanza jana na wawezeshaji ni wataalamu kutoka OUT na SADC.

Alisema OUT walipata nafasi ya kutoa mafunzo hayo baada ya kuzishinda nchi wanachama ambapo michuano hiyo ilifanyika mwaka 2009 na Dola milioni moja za Marekani zitatumika kutoa elimu hiyo.

“Fedha hizo tumezipata kama msaada kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kupitia SADC kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kwa nchi wanachama ambapo mafunzo hayo hutolewa kila baada ya miaka mitatu kwa vyuo kushindanishwa,” alisema Profesa Mbwete.

Alisema katika mafunzo hayo, kila nchi imeleta watu wanne kwa ajili ya kujifunza elimu hiyo na wana imani baada ya kumaliza mafunzo hayo wataenda kuwafundisha na wenzao.

Alisema wataanza na kozi fupi na baadaye kozi ndefu kwa wanafunzi kutoka SADC watasoma mambo yanayohusiana na mambo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Alisema baada ya kumaliza mafunzo hayo watakuwa na kozi nyingine tisa na amewataka Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kuacha kubweteka kuwaachia wageni kwa kuwa lengo la Tanzania ni kuwasaidia wananchi.

Alizitaja nchi zinazoshiriki mafunzo hayo kuwa Namibia, Tanzania, Afrika Kusini, Botswana na Lesotho.

NA MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top