WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira,
amepinga vikali madai yaliyotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles
Lema (Chadema) akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete ndiye muasisi wa udini.
Akizungumza bungeni jana, Wassira alimshangaa Lema kwa kutoa kauli hiyo,
ambayo alisema imemvunjia heshima rais na kwamba hiyo ni kinyume cha
Katiba.
“Mimi nimesikitishwa sana na kauli ya Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyoitoa jana (juzi) humu ndani akisema Rais Kikwete ndiye mwasisi wa suala la udini.
“Nimeshangazwa kwa sababu tuhuma hizi dhidi ya mkuu wa nchi ni nzito hazipaswi kusemwa tu hivi hivi, mimi nafikiri hili Bunge sasa sijui tunakwenda wapi.
“Kwa maneno haya Lema amevunja Katiba kwa kusema makali kiasi hiki dhidi ya rais, tunataka Lema alete ushahidi juu ya tuhuma hizi.
“Rais anapoteua wakuu wa mikoa na wilaya anashauriana na waziri mkuu ambaye huyu tuliyenaye leo ni mkiristo.
“Anapoteua makatibu wakuu anashauriana na katibu mkuu kiongozi, Ofisi ya Rais ukimwondoa yeye mwenyewe waliobaki wote ni Wakristo. Huo udini uko wapi?
“Lema lazima ajue kuna hotuba za kijiweni na hotuba za bungeni lazima atofautishwe, lakini hapa kinachofanyika watu wanaleta hotuba za kijiweni badala ya hotuba za Bunge.
“Mgogoro wa kuchinja, mimi nilikwenda kule Geita kwenye mgogoro tukamaliza huu mgogoro kwa kuwashirikisha waumini wa dini, nashanga Lema anasema Serikali haijachukua hatua yoyote.
“Namtaka Lema popote alipo ajue kwamba Serikali inafanya kazi kwa utaratibu, alitaka tuende pale tutoe amri, asubiri atakapoingia madarakani sijui ni lini ndipo aendeshe Serikali kwa amri tu bila kushirikisha watu
Wassira alikuwa akihitimisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi) ambapo alisema hisia za udini nchini zimechochewa zaidi kupitia mikanda (CD) mbalimbali ya kidini.
Alisema Kanda hizo zilikuwa zikihamasisha na kuwataja viongozi na maaskofu wa Kikristo, lakini zote zimekamatwa na serikali imeahidi kuwalinda viongozi hao.
Alisema kanda zote zimekamatwa na yeyote mwenye nazo akikamatwa atachukuliwa kuwa ni mchochezi sawa na waliotengeneza kanda hizo.
“Wale waliokimbilia nje ya nchi tunaendelea kuwatafuta kwa kutumia polisi wa kimataifa (Interpol) ili waje kujibu kesi ya uchochezi.
“Mheshimiwa Spika, hata hivyo udini unaoenezwa bado haujavuruga maisha ya wananchi, kwamba wananchi huko mitaani wanaendelea kushirikiana vizuri, hakuna kubaguana. Na nadhani tatizo halijawa kubwa kupindukia.
“Suala la udini linakuzwa zaidi na watu wenye malengo mabaya ya kisiasa, tangu huko nyumba hata Zanzibar yenye asilimia zaidi ya 90 waislamu haijawahi kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi ya kiislamu.
“Udini ulichochewa na wanasiasa mwaka 2010 kwa sababu ya watu kutaka madaraka. Mwaka huo haukuwa mzuri sana, lakini tuyaache, yaliyopita si ndwele.
“Wahenga walisema, usipoziba ufa utajenga ukuta, baba wa taifa, hayati Mwalimu Nyerere alisema ukisikia wanaopaza zaidi sauti za udini ndiyo wanaoueneza, kwa hiyo tuwe makini na wanaopiga kelele juu ya jambo hilo.
“Katika suala hili, ni vema Bunge litafute namna bora ya kushughulikia suala hili ili lisiendelee kuwa kikwazo kwa amani ya nchi yetu” alisema Wassira

Usalama wa taifa
Mbali na suala hilo, Wassira pia alionyesha kuchukizwa na tuhuma nzito zinazotolewa hivi sasa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa, ikihusishwa na vitendo viovu vya utekaji na utesaji watu.
Wassira alisema si kweli kwamba idara hiyo ina kazi ya kutesa watu kwa kuwanyofoa kucha, meno na utesaji mwingine kama inavyodaiwa na wapinzani.
Alisema ni vema Watanzania wajue kuwa kila nchi duniani inao usalama wa taifa kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa husika na si kutesa watu kama wanavyotaka kuwaaminisha.
Alisema usalama wa taifa ni tofauti na polisi kwa sababu wanafanya kazi chini kwa chini, na kwa kiasi kikubwa uliwahi kusaidia kuzima njama za uhaini, na uhalifu katika mabenki mwaka 2005.
“Hivi watu hawa tena, badala ya kulinda watu waanze kuondoa vidole vya watu. Hata hayo mambo ya ugaidi ambayo yanafanyika nchi zingine, kushambuliwa kwa ubalozi wa marekani, usalama walifanya kazi nzuri.
“Si kweli kwamba wanaweza kumtesa Kibanda, Mhariri Mtenaji Mkuu wa New Habari 2006.
“Afadhali vitendo hivyo vingewakuta Mbowe au Dk Slaa ambao ni wapinzani wa Serikali, lakini tufanye hivyo kwa Kibanda ili iweje?
“Sipingani na vyama vya siasa kuwa na mkakati wake, sisi wote nikutoka vyama vya siasa lazima tuwe na mikakati ya kuchukua dola. Chadema wanayo operesheni Sangara, na sasa M4C sijui kama nayo imekufa, hiyo hatuikatai.
“Lakini kama unafanya kazi kwa kuhatarisha amani kwa kufanya maandamano na kutaka kuharibu amani ya nchi lazima idara ya usalama wa taifa itakufuata.

NA MTANZANIA
Post a Comment