TAWI LA CCM WASHINGTON DC, MARYLAND& VIRGINIA
Chama cha Mapinduzi tawi la Washington DC, Maryland na Virginia,
tumesikitishwa na tukio la mlipuko siku ya Jumapili, Mei 5 2013 mjini
Arusha.
Chama cha Mapinduzi tawi la DMV tuna laani vikali shambulio hilo
lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya kwa
Taifa letu la Tanzania. Tukio hilo la kusikitisha limepoteza mtanzania
mwenzetu na kusababisha wengine 40 kupata majeraha na maumivu makali.
Tunaamini serikali itafanya kazi yake ya kuwasaka wahusika na wote walioshiriki kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Tunatoa rambi rambi kwa watanzania wenzetu walioathirika kwa kuondokewa
na wapendwa wao na wale wote waliopatwa na majeraha katika tukio hilo.
Mwenyezi mungu awape nafuu ili warejee kwenye shughuli zao za kila siku.
Mungu ibariki Tanzania
UONGOZI WA TAWI LA CCM
WASHIGTON DC, MARYLAND NA VIRGINIAMAREKANI
Post a Comment