Ali Zeidan alitekwa nyara na kundi la waasi waliokuwa na uhusiano na serikali kwa jina Revolutionaries Operations Room.
Walisema walimteka nyara kwa maagizo ya mwendesha mkuu wa mashtka ingawa wizara ya sheria imekanusha madai hayo.
Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi ya wapiganaji walioghadhabishwa na hatua ya makomandao wa Marekani kumkamata Anas Al-Liby mshukiwa wa kundi la kigaidi la al-Qaeda.(P.T)
Wengi walitaja hatua ya Marekani kama
ya kuingilia uhuru wa taifa hilo na kata kutaka maelezo kutoka kwa
balozi wa Marekani nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.
Serikali imekuwa ikikabiliwa na
shinikizo kali baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa
viongozi wa al-Qaeda Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini
Tripoli kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa
dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.
Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa
Marekani na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha
vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi
yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo
mengine ya kanda hiyo.