Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi
mbalimbali wa CCM waliofika kumlaki alipowasili kwenye eneo maarufu
linalojulikana kama Nonga Nonga wilaya ya Songea mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na
waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu
Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa
kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa
harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazee waasisi pamoja na
wananchi wa kata ya Matogoro ambapo alitaka wana CCM kuenzi kazi
zilizofanywa na waasisi wetu kwa kudumisha mshikamano ,umoja na amani.
Ofisi ya Kata ya Matogoro CCM ambayo
iliwekwa jiwe la msingi tarehe 20 Desemba 1986 na Mzee Rashid Mfaume
Kawawa,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi kutoa bati
za kuezeka ofisi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana akihutubia wananchama wa Shina namba 1tawi la Ambachai kata ya
Mfaranyaki nyumbani kwa Balozi wa Shina Ndugu Magreth Mchula,Katibu Mkuu
alisisitiza viongozi wa ngazi za chama kuwa na mazoea ya kutembelea
mabalozi wao kwani ndio msingi wa wanachama.
Wanachama
wa Shina namba 1 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana,pichani Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa
amejumuika na wanachama kukaa nao pamoja kwenye mkeka.
Mzee
Mustafa Mohamed Songambele akionyesha furaha yake alipokutana na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mfaranyaki Songea,Katibu Mkuu
ameanza leo ziara ya kuetembelea wilaya ya Songea mjini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Tanu na mwanasiasa wa muda mrefu.
Mlevi wa Vijana wajasiriamali wa
Mfaranyaki Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu vijana hao baada ya
kufunguliwa kwa Shina lao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana.