|
Na
Ally Kondo, Kuwait
Serikali
ya kuwait imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni moja (1) kwa ajili ya
kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu katika kipindi cha miaka
mitano ijayo. Tangazo hilo lililotolewa na Amir wa Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano baina ya Nchi za
Afrika na Kiarabu (Third Afro Arab Summit), Sheikh Sabah Al-Ahnad Al-Sabah
wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi ya mkutano huo nchini Kuwait siku ya
Jumanne tarehe 19 Novemba, 2013.
Sanjari
na kiasi hicho cha fedha, Sheikh Al-Sabah alitangaza kiasi kingine cha Dola za
Marekani milioni moja (1) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za utafiti
zenye lengo la kuibua fursa za maendeleo katika nchi za Afrika.
Sheikh
Al- Sabah aliwambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, Mkutano wa Tatu wa Afro Arab
Summit unafanyika huku nchi nyingi za Afrika na Kiarabu zikikabiliwa na
changamoto za kisiasa na kiuchumi ambazo bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu
malengo yanaayowekwa katika mikutano hiyo hayatafikiwa. Alisisitiza nchi za
Afrika na Kiarabu kuwekeza katika miradi itakayoimarisha ushirikiano wao
akitolea mfano wa sekta ya kilimo. “Endapo usalama wa chakula hautakuwa wa
kuaminika katika nchi za Afrika na Kiarabu, kutazifanya nchi hizo kuwa katika
hali tete na hatimaye kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi wao. Sheikh
Al-Sabah alisikika akisema.
Aidha,
Amir wa Kuwait aliwaomba Wakuu wa Nchi kutumia mkutano huo kutafuta suluhu ya
kudumu ya mgogoro unaoendelea nchini Syria ambao athari zake unaikumba kanda
nzima ya Kiarabu. Alihitimisha hotuba yake kwa kulitolea wito Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Israel itekeleze Maazimio ya Umoja wa Mataifa
kuhusu Mamlaka ya Palestina.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe.
Hailemariam Dessalegn alieleza kuwa nchi za Afrika haziwezi kufikia mapinduzi
ya kijani endapo hakutawekwa mkazo katika sekta za nishati jadilifu,
miundombinu na utalii. Hivyo, alisisitiza umuhimu wa mkutano huo kubuni
mwongozo makini wa ushirikiano utakaowezesha kufikiwa kwa malengo hayo.
Mhe.
Dessalegn alizihimiza nchi za Afrika na Kiarabu kuongeza nguvu mara dufu katika
mapambano dhidi ya uharifu wa mipakani, ugaidi, uharamia pamoja na uhamaji wa
kinyume cha sheria. Aliweka angalizo kuhusu tatizo la uhamaji kwa kusema kuwa
endapo halitafanyiwa kazi vizuri linaweza kudhoofisha ushirikiano huo. Hivyo,
aliunga mkono pendekezo la kuunda Kamati ya Pamoja ya Wataalamu kutoka nchi za
Afrika na Kiarabu ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Mwenyekiti
wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosazana Dlamini-Zuma naye
aliwahakikishia Wakuu wa Nchi katika mkutano huo kuwa, Afrika imejizatiti
kutekeleza yale yote mazuri yatakayoafikiwa katika mkutano huo. Aidha,
alihimiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu ili idadi kubwa ya vijana ambao ndio
nguvu kazi na wanawake ambao ni zaidi ya nusu katika nchi za Afrika wapate
elimu bora inayoendana na madadiliko yanayotokea duniani hivi sasa.
Ujumbe
wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu
wa Rais ambaye pia amepangiwa kutoa hotuba.
|
|
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal wa pili kutoka kushoto akisikiliza ahadi ya Amir wa Kuwait ya
kuzikopesha nchi za Afrika Dola za Marekani biliomni moja. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abdillah Omar wa kwanza
kushoto, Mbunge wa Wawi, Mhe. Ahmadi Rashidi na Mbunge wa Gando, Mhe.
Khalifa Khalifa nao walishuhudia ahadi ya Amir wa Kuwait. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz mwenye ushungi mwekundu na
kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara
ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya nao walikuwepo katika ukumbi wa
mkutano wakati Amir wa Kuwait akitoa hotuba. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Biashara
on Wednesday, November 20, 2013