Asema atakuwa wa mwisho kutoka kwa hiari yake, atoa majibu ya tuhuma sita
Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema kuwa hana mpango wa
kujiondoa Chadema na kusisitiza kwamba atakuwa mtu wa mwisho kujitoa
ndani ya chama hicho kwa hiari yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana katika mkutano aliouandaa kwa pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati
Kuu, Dk Kitila Mkumbo, Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alisema kwamba
amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa na umri wa miaka 16 hivyo
haiyumkiniki akikimbia chama hicho.
Zitto na Dk Kitila walivuliwa nyadhifa zao wiki iliyopita wakihutumiwa kukihujumu chama hicho.
“Kuna watu ambao walitegemea kuwa leo hii
ningejibu mapigo, ‘ningezodoa,’ watu wengine kwa majina kama ilivyo
kawaida kwa siasa za Tanzania. Natambua pia kama ilivyo kawaida wakati
wa migogoro kwa vyama hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo
ningetangaza kinachoitwa ‘maamuzi magumu’,” alisema na kuongeza:
“Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia
nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu,
napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia wote nchini watambue
kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa
mwisho kutoka kwa hiari yangu.”>>>>>Endelea kusoma hapa