Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi anatarajiwa kutua leo mchana majira ya saa 9:30 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda.
Hii ni taarifa rasmi kwa wapenzi wa soka, wanacham na mashabiki kuwa
rasmi mchezaji huyo atawasili leo na kupokelewa na viongozi wa klabu ya
Yanga pamoja na mashabiki na wanachama kwa ujumla.
Ujio
wa Emmanuel Okwi leo unafuatia kukamilisha masuala yake yaliyokuwa
yamembakisha nchini Uganda na moja kwa moja leo ataungana na wenzake kwa
ajili ya maandalizi ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba SC katika Nani
Mtani Jembe.