Klabu ya Young Africans SC imeingia
mkataba wa kurusha mchezo wake wa hatua ya kwanza ya mashindano ya klabu
Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Alh Ahly ya Misri kwa gharama ya dola za
kimarekani elfu 55,000 sawa na mil 90/= za kitanzania kwa muda wa
dakika 90.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Young
Africans Katibu Mkuu Bw. Beno Njovu amesema wameingia mkataba huo na
kampuni ya SGM kutoka nchini Ufarans na moja kwa moja wameipa uwakala
kampuni ya MGB ya Zamaleki ya Cairo.
Mkataba huo unawapa kibali
kampuni ya SGM kurusha moja moja mchezo mchezo wa Yanga dhidi ya Al Ahly
utakaofanyika Tanzania nchini Misri, nchi za Afrika Kaskazini na
Mashariki ya Mbali huku pia vituo vya telesion vya ndani ya nchi
vikipewa fursa ya kuonyesha ndani ya nchi.
SGM imefikia hatua hiyo
kufuatia kuona ratiba ya Klabu Bingwa Afrika iliyotoka mwanzoni mwa
wiki kuonyesha kuwa timu ya Young Africans itaanza na timu ya Komoronize
katika hatua ya awali na kisha kukutana na Al Ahly katika hatua ya 32
bora.
Mwakilishi wa SGM Bw. Francis Gaitho amesema wao wameamua
kuingia makubaliano hayo na Yanga mapema wakiwa na uhakika kuwa timu ya
Yanga itasonga mbele katika hatua ya awali na hivyo watakutana na
mabingwa watetezi Al Ahly.
Yanga
itaanza kucheza na timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro Februari 8
mwakani uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana nao wiki
baadae nchini kwao Comoro na kikifanikiwa kuvuka hatua hiyo ndo
itakutana na Al Ahly Februari 28, 02, 02 Machi na kurudiana baada ya
wiki moja nchini Misri.