Pluijm raia wa Uholanzi, alitua katika mchezo huo akiwa na peni na
karatasi akiwa na kiongozi mmoja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema jambo
lingine lililomshangaza katika kikosi cha Simba ni uwezo wa Messi na
Kiemba ambao kwake wanahitaji kuchungwa sana.
,,,,,,,,,,,,,,,,
MZUNGU wa Simba, Zdravko Logarusic aliibuka kimyakimya Jumamosi
kuangalia Yanga ikicheza na Ashanti, akasoma ufundi wa kocha mpya wa
Jangwani, Hans Pluijm na kuishia zake.
Logarusic aligoma kutamka chochote alichokigundua
kwenye staili ya soka la Yanga mpya ya Pluijm ambaye ni kama mtani wake
kwa vile wanajua vilivyo ndani na nje ya uwanja.
Lakini siku inayofuata Pluijm naye akaibuka Taifa
kuiangalia Simba ambayo hakuwahi kuiona tangu asaini Yanga. Unajua
alichosema? “Mbona wanacheza nyuma ya mpira tu?” Lakini mechi
ilipomalizika akaondoka na jina la Ramadhan Singano ‘Messi’ na Amri
Kiemba kwenye kitabu chake.
Akizungumza na Mwanaspoti wakati akiishuhudia
Simba ikiiangamiza Rhino ya Tabora kwa bao 1-0, juzi Jumapili katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Pluijm alisema ameuangalia mchezo
huo, lakini amebaini kwamba Simba inajilinda zaidi kama ilivyokuwa kwa
Rhino kitu ambacho hakikumvutia hata kidogo.
Pluijm raia wa Uholanzi, alitua katika mchezo
huo akiwa na peni na karatasi akiwa na kiongozi mmoja wa Yanga, Hafidh
Saleh, alisema jambo lingine lililomshangaza katika kikosi cha Simba ni
uwezo wa Messi na Kiemba ambao kwake wanahitaji kuchungwa sana.
Alisema kwa upande wa Messi ni nyota muhimu Simba
ambaye ni msumbufu kwa mabeki na ana uwezo wa kuzuia wachezaji wa timu
pinzani wasipande kusababisha madhara kwa Simba huku Kiemba akimuelezea
kwamba anajiamini na anatoa pasi za uhakika.
“Sikuona soka ya kuvutia sana, ilipooza hakukuwa
na mpira wa presha, Simba inacheza taratibu na inajilinda sana ndiyo
maana mpira haunogi,”alisisitiza kocha huyo na kudai kwa ukubwa wa Simba
ilipaswa kushambulia si kujilinda.
“Nimefurahishwa sana na uwezo wa yule mwenye namba
11(Messi) mgongoni ni hatari sana anastahili ulinzi muda wote, hata
yule namba 28 (Kiemba) yuko vizuri sana,”alisema.
Kocha huyo wa Yanga alikuwa hajaiona Simba awali
kwani aliposaini mkataba na Yanga alikwenda moja kwa moja kambini
Uturuki hadi aliporejea wiki iliyopita. Makocha hao wanajuana vilivyo
kwani wamewahi kufanya kazi kwenye timu tofauti katika Ligi ya Ghana.
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic alikuwa uwanjani
kuiangalia Yanga ikicheza na Ashanti United lakini hakutamka lolote
kuhusiana na mabadiliko aliyoyaona kwa kocha mpya wa Jangwani.
CHANZO:Mwanaspoti
CHANZO:Mwanaspoti
