 |
| Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano kuhusu masuala ya
Uhamiaji na Watanzania waishio nje (Diaspora). Ufunguzi huo ulifanyika
katika Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari,
2014. Wengine katika picha ni Bw. Damien Thuriaux (kulia), Mkuu wa
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) hapa nchini na Bw. Jo Rispoli,
Mtaalam wa masuala ya Uhamiaji katika Shirika hilo. |
 |
| Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kongamano hilo wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) |
 |
| Bw. Damien naye akizungumza huku Mhe. Membe akimsikiliza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo |
 |
| Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akifuatilia kwa makini
ufunguzi wa kongamano kuhusu masuala ya Diaspora. |
 |
| Wajumbe
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Kutoka kulia ni Bw. Seif Kamtunda,
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Linda Helgesson, Mtaalam wa masuala ya Maendeleo
ya Wahamiaji, Bi. Sudah Lulandala, Afisa Mipango na Bi. Tunsume
Mwangolombe, Afisa Mambo ya Nje. |
 |
| Picha ya pamoja. |
 |
Mhe. Membe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ufunguzi wa kongamano hilo.
Na Reginald Philip
Kisaka
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard K. Membe (Mb) amesisitiza umuhimu wa Tanzania kuridhia uraia wa nchi
mbili ili Watanzania wanaoishi ughaibuni waweze kufaidika na fursa za kiuchumi
na kijamii zinazotolewa kwa raia katika nchi wanazoishi.
Mhe. Waziri alitoa kauli hiyo katika ufunguzi wa kongamano
lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na kufanyika katika
Hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2014. Kongamano
hilo ambalo linawakutanisha wawakilishi kutoka Serikalini, wanazuoni, asasi za
kiraia na watafiti mashuhuri lina lengo la kujadili njia mbalimbali ambazo
wanadiaspora wanaweza kuzitumia kuchangia maendeleo ya nchi yao kwa mazingira
ya Tanzania.
Mhe. Waziri aliwambia wajumbe wa kongamano hilo kuwa hoja ya
uraia wa nchi mbili itawasilishwa na kutetewa katika Kikao Maalum cha Bunge la
Katiba ambacho kinatarajiwa kufanyika katika siku za karibuni. “Endapo uraia wa
nchi mbili utaridhiwa, Watanzania wanaoishi ughaibuni wataweza kupata kazi
nzuri na kukopa benki katika nchi
wanazoishi, hivyo kipato chao kitaongezeka ambacho watakitumia pia kuwekeza
nyumbani. Mhe. Waziri alisikika akisema.
Mhe. Membe alibainisha kuwa nchi zilizoridhia uraia wa nchi
mbili na kuweka mazingira mazuri ya wanadiaspora katika kuchangia maendeleo ya
nchi zao na kuchangia pato la taifa ni pamoja na Nigeria, Ghana na Kenya.
Awali, akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kongamano hilo, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji hapa nchini Bw. Damien
Thuriaux alisema kuwa, kongamano hilo ambalo litafanyika kuanzia tarehe 22 hadi
29 Januari 2014 lina lenga kuhamasisha uratibu wa masuala ya Uhamiaji na
Diapora kwa kuzishirikisha Wizara na Taasisi mbalimbali. Aidha katika
kushirikiana na Serikali ya Tanzania, Bw. Damien alisema kuwa Shirika lake
litasaidia uundwaji wa Tovuti maalum kwa ajili ya watu waishio Nje (Diaspora)
na masuala mengine yanayohusu uhamiaji. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Siasa
on Thursday, January 23, 2014