Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

JAGUAR KIOO (OFFICIAL VIDEO)

DAKIKA 45 ITV:SIKILIZA AUDIO YA MAHOJIANO YA DAKIKA 45 YA ITV NA JAJI WARIOBA

Katika kipindi cha mahojiano ya dakika 45 ITV leo hii kimepata fursa ya kufanya maongezi na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba...Via ITV SOURCE:SWAHILIVILLA

TASWIRA:SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

  Ndege za kivita nazo zikipita angani .
 Mwanajeshi akitua na mwanvuli kutoka angani mita 4000 kutoka usawa wa bahari

 Baadhi ya zana za  kivita za kisasa zikipitishwa mbele  ya Mhe. Rais Kikwete na wageni waalikwa ikiwa ni moja ya kusherehea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kikosi cha Makomando wakionesha mbele ya Mhe. Rais, wageni waalikwa na wananchi mafunzo waliyopitia
 Watoto wa Halaiki wakionesha umbo la picha za Rais wa Kikwete na Rais Shein na maneno yanayosomeka Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Watoto kutoka Tanzania Bara na Zanziba wakionesha utaalamu wa kucheza ngoma
Kikundi cha Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum wa pamoja kuhusu miaka 50 ya Muungano.
Picha Reginald Philip na Ofisi ya Makamu wa Rais

TASWIRA:SIKU YA KUKUMBUKWA MUUNGANO

Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akiwa ameruka kwa miguu yote hewani na kuvunja mbao zilizokuwa zimeshikwa na wenzake wakati wa maonyesho ya kijeshi ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. 
Picha na Emmanuel Herman

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAFURIKO MKOA WA PWANI


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakikagua athari za mafuriko zilizoharibu vibaya barabara ya Chalinze- Dar es Salaam eneo la Ruvu Darajani leo.Mamia ya abiria walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo.Picha na Freddy Maro-IKULU

TAHADHARI DHIDI YA UHALIFU UNAOFANYWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof John Nkoma
---
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kuzingatia kifungu 5 (b) na (e) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya 2003 inatoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, wananchi na umma kwa ujumla kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kama ifuatavyo:

1. Usimpe mtu yeyote usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.

2. Usitoe maelezo yoyote kuhusu namba yako ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu yeyote anayekupigia simu kutaka taarifa hizo.

3. Usijibu ujumbe wa simu unaohusiana na fedha zako hata kama namba iliyotuma unaifahamu.

4. Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwenye namba ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe uzungumze naye.

5. Usitekeleze maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaokutaka kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kwamba simu yake ina hitilafu hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.

6. Ukipata ujumbe kwamba umepokea fedha kwa njia ya simu, mpigie aliyekutumia na usitoe pesa hizo hadi uthibitishe kwamba zimetumwa kwa nia njema.

7. Weka njia za kuthibitisha taarifa kabla ya kufanya miamala ya kifedha kutumia simu ya mkononi.

8. Ukipigiwa simu na mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani unamfahamu mtu huyo; mpigie tena kwa namba yake unayoijua ili kuhakikisha kwamba ni yeye.

9. Iwapo unafanya biashara ya huduma za simu hakikisha kwamba simu unayoitumia kwa miamala ya kifedha ni tofauti na unayotumia kwa shughuli nyingine na hakikisha simu hiyo haitumiwi na mtu mwingine

10. Tumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia.

11. Usitoe namba zako za siri unazotumia kwa huduma

12. Thibitisha na hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma

13. Ukipoteza simu au laini yako ya simu toa taarifa kwa mtoa huduma wako na Polisi mara moja.

14. Ukifanyiwa uhalifu ambapo simu au mtandao umetumika kufanyia uhalifu huo hilo nikosa la jinai. Toa taarifa Polisi ili wahalifu wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

15. Usipopata ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma wako katika kutatua tatizo lako wasilisha malalamiko yako Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kutuandikia ( S.L.P 474 Dar es Salaam); kufika ofisini makao makuu namba 20 Sam Nujoma Dar es Salaam au kwenye ofisi za Kanda na Zanzibar; kupiga simu ( namba 0784 558270 au 0784 558271) na kwa barua pepe (malalamiko@tcra.go.tz au complaints@tcra.go.tz)

Imetolewa na:
 MKURUGENZI MKUU
 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

LIVERPOOL WAZIDI KUJIKITA KILELENI


WHY EDUCATION MANAGEMENT, HUMAN RESOURCES IN SHAMBLES


Professor Issa Omari
Professor Issa Omari of The Open University of Tanzania (OUT) gives a highlight of his new book titled ‘Education Sector Human Resources and Management Crisis in Tanzania.’  He comes out with reasons as to  why the status of Education is in shambles and suggests how the crisis can be overcome as he speaks to The Guardian Staff Writer, Michael Haonga in this interview. Excerpts.. .
 
QUESTION: May you first acquaint readers of this interview with your CV?
ANSWER: I am a holder of Bachelor of  Arts in Economics with Education degree (1968):  a Bachelor Philosophy -Educational Measurements, (1969); MA-Educational Psychology  and PhD (1972). Currentlly Professor Emeritus at Open University of Tanzania. I teach research methods, psychology, and educational assessment . I have been a professor since 1978.
 
Q: What is the magnitude of the crisis, its causes and  impact in short and long- term aspects?
A: The crisis is not just big but huge bordering a calamity and is an accumulation of errors of judgment and negligence for over a decade now. Can you imagine a country where universities do not get enough students especially in the sciences; over 180 secondary schools close down in two years for lack of students; over 90 percent of students fail Form Four examinations; Participation rates are below five percent at A level, and in higher and tertiary education levels; Children refuse to go to school to sit on puddles, and schools have no teachers, books, and desks.
 
Q:  What are your proposals to deal with the crisis?
A: First you need political appreciation of the magnitude of the problem, and then commitment, followed by additional resources. Tanzania is spending very little on education and paying teachers lowest in the continent.  Secondly you have to have more inspiring and relevant leadership in the education sector. Special attention is required to improve the supply of qualified school candidates and teachers in the sciences if the future of the economy is to be secure.
 
Q. What do you suggest to be prioritized in dealing with the crisis and why?
A: Quality of the leadership in the sector: Quality of teaching force, and then the study and living conditions at the school level. 
 
Q:  Whom does the book target? 
A: Yes, once books are published, they are public commodities for those interested. For strategic persons, such as directors they can get complementary copies but for the rest, 20,000 shillings is not too much to ask.
 
Q: What have you to comment on the general trend of education in Tanzania?   
A: There has been an extremely dangerous silence about the fate of the education enterprise in Tanzania. One day workshop on the findings and recommendations should help us to move forward in tracking the crisis.
 
SOURCE: THE GUARDIAN
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top