Halima Mdee akielekea kupanda gari la
Polisi kuelekea Gereza la Segerea huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi jana baada ya kukosa dhamana
---
Mbunge
wa Kawe- Chadema, Halima Mdee na wenzake 8 jana wamepata dhamana katika Mahakama
ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku
ya juzi washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi
Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu,
Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi,
Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward
Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee
na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa
wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni,
walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka
watawanyike.
Shtaka
la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa
ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na
sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.
Hisani ya HakiNgowi Blog.
Post a Comment