Kuanzia leo longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp
itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa
mchana kweupe.
- Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
- Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
- Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
- Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
- Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
Kuanzia jana huduma hiyo inayomilikiwa na
Facebook- itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini
kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.
Chanzo:Taarifa
Post a Comment